• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

RAIS MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI

Posted on: December 2nd, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli leo ameweka jiwe la msingi katika mradi wa maji safi na usafi wa mazingira wa jijini Arusha katika kata ya Kimnyaki wilayani Arumeru.

Amesema wananchi wote ambao wanaishi katika vyanzo vya maji na ambao mradi utawapitia katika maeneo yao watapatiwa maji kwanza wao kabla yakusambazwa maeneo mengine.

Magufuli amesema mradi huu ambao utawanufaisha wananchi wa jiji la Arusha kwa kiasi kikubwa lakini hata pia wananchi wa kata ya Oldonyosambu wilayani Longido pia nao wapatiwe maji kutoka kwenye mradi huo.

“Jana nimesimamishwa  njiani na wananchi wa Oldonyosambu na kero yao kubwa ilikuwa ni ukosefu wa maji safi kwani wanayoyatumia sasa yama madini ya Floride kwa wingi hivyo yanawaadhiri sana wao na watoto wao.”

Amesema fedha zilitumika katika ujenzi wa mradi huo wa maji ni mkopo wa riba nafuu kutoka Benk ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), hivyo wananchi wote wanajukumu la kulilipa deni hilo.

Magufuli amewataka wakandarasi wa mradi huo ambao wapo 10 wafanye kazi kwa bidii usiku na mchana ili kuhakikisha mradi unakamilika ifikapo mwanzoni mwa Juni 2020 na wananchi waweze kupata maji kwa haraka.

Waziri wa maji na umwagiliaji Pro Makame Mbalawa amesema, hitaji la maji kwa mkao wa Arusha ni lita milioni 94 kwa siku lakini mradi huo unauwezo wakuzalisha lita milioni 208 kwa siku hivyo  ni zaidi ya mara 4 ya uhitaji wa Mkoa.

Akisoma taarifa ya mradi huo Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya maji safi na taka Arusha Enginia Ruth Koya amesema, mradi huo hadi kukamilika utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 520.

Amesema mradi huo utakuwa na uwezo wa kuzalisha lita milioni 208 kwa siku tofauti na hali ya sasa ambayo ni lita milioni 40 kwa siku huzalishwa sawa na asilimia 42 na hitaji la mkoa ni lita milioni 94 kwa siku.

Koya amesema kutokana na ongezeko hilo la uhitaji wa maji wa takribani asilimia 100 hadi ifikapo 2020 mkoa wa Arusha utakuwa na uwezo wakuwahudumia watu takribani milioni 1.

Mbali na mafanikio hayo amesema changamoto kubwa wanayokutana nayo ni ugumu wa kupata njia zakulaza mabomba hasa katika maeneo ambayo hayajapimwa,pia gharama kubwa za fidia wanazopaswa kuwalipa wananchi.

Rais Magufuli amefanya ziara yake katika mkoa wa Arusha kwa siku 2 kuanzia Desemba 1 hadi Desemba 2,2018 nakuweza kufungua kituo cha malipo ya forodha cha pamoja Namanga wilayani Longido na kumalizia na uwekaji jiwe la msingi katika mradi mkubwa wa maji safi na mazingira wa jijini Arusha.

Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2022 January 29, 2023
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2023 December 14, 2022
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • MAADHIMISHO YA MIAKA 2 YA MAMA SAMIA AKIWA MADARAKANI

    March 19, 2023
  • BONANZA LA MIAKA MIWILI YA MAMA SAMIA

    March 18, 2023
  • UZINDUZI WA KITABU CHA MIAKA MIWILI YA DKT.SAMIA

    March 14, 2023
  • TUMERIDHISHWA NA MIRADI-KAMATI YA SIASA MKOA

    March 09, 2023
  • Angalia Zote

Video

THE ROYAL TOUR
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa