Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Missaile Albano Musa amefika kituo cha Mahakamani AICC kata ya Sekei na kuboresha taarifa zake kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga kura mapema leo Desemba 17m 2024, ikiwa ni Maandalizi ya Uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unafanyika Mkoani Arusha, Kilimanjaro na mkoani Dodoma kwenye Halmashauri za Wilaya ya Kondoa, Chemba na Mji wa Kondoa kuanzia tarehe 11 hadi 17 Desemba, 2024 ambapo vituo vinafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa