Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Missaile Albano Musa ameiagiza halmshauri ya Arusha kuongeza kasi zaidi katika kukusanya mapato na madeni sambamba na utekelezaji wa Miradi kwa Wakati.
Maagizo hayo yametolewa na Katibu Tawala huyo kwenye kikao cha kupitia hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) kwa mwaka 2022/23.
Aidha, amesisitiza lazima ukusanyaji wa mapato uongezwe ili kuhakikisha madeni yote yanayodaiwa na wazabuni, watumishi ikiwemo miradi ya maendeleo kwa wananchi Kutekelezw.
"Hongereni kwa kupata hati safi lakini nawasihi mjikite zaidi katika ukusanyaji wa mapato sanjari na ulipaji wa madeni na utekelezwaji wa miradi iliyopo". Amepngeza Katibu Tawala.
Naye Diwani wa Kata ya Olmotinyi, Mhe. David Kinisi amehoji ni kwanini vifaa tiba vilivyonunuliwa na Serikali kwa zaidi ya shilingi milioni 300 kama x-ray , vifaa vya maabara viwepo katika vituo vya afya kwenye halmshauri hiyo lakini vinashindwa kufanya kazi kwasababu ya ukosefu wa umeme.
Ambapo Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo, Dkt. Japhet Champanda amekiri uwepo wa vifaa tiba hivyo kwenye baadhi ya vituo vya afya lakini changamoto kubwa ni ukosefu wa umeme na kuomba Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Arusha kupeleka umeme kwenye baadhi ya vituo vya afya na zahanati ili huduma za afya zinazostahiki kutolewa kwa wananchi ziweze kutolewa.
Awali Mwekahazina wa Halmashauri hiyo, Tiddo Morio amesema halmshauri hiyo inajumla ya hoja 29 kwa mwaka wa fedha 2022/23 ambapo hoja 20 zimefungwa ya kubaki na hoja tisa .
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa