• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

RAS ARUSHA: WALIMU SIMAMIENI WANAFUNZI KATIKA  MASOMO NA UTUNZAJI WA VIFAA VYA SHULE..

Posted on: November 29th, 2023

.Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Missaile Albano Mussa, amewataka walimu wa shule za Msingi mkoani humo,  kuwasimamia wanafunzi katika masomo ili kupandisha kiwango cha ufaulu, pamoja na utunzaji wa vifaa vya shule, ikiwemo miundombinu.


Mussa ameyasema hayo wakati akizungumza na walimu wa shule za Msingi Kaloleni na Nasholi, Halmashauri ya Meru, Mkoa wa Arusha, mara baada ya kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa, mradi uliogharimu kiasi cha shilingi milioni 106.2, kupitia program ya BOOST.


Amesema kuwa walimu wanalo jukumu kubwa la kuwasimamia wanafunzi katika masomo ili waweze kufaulu vizuri, kusimamia nidhamu pamoja na utunzaji wa vifaa vyote vya shule, ikiwemo miundombinu, kwa kuwa, serikali inafanya kazi kubwa ya kuwezesha uwepo wa mazingira bora ya ufundishaji kwa walimu na ujifunzaji kwa wanafunzi, ikiwemo ujenzi wa miundombinu bora kwenye shule nchini.


“Serikali imefanya sehemu yake ya kuwekeza miundombinu bora na rafiki shuleni, kazi iliyobaki tunawategemea ninyi walimu, kuwasimamia watoto wetu, kuwa na nidhamu, uadilifu na kujituma ili waweze kufaulu vizuri, kwa manufaa ya Taifa letu” amesisitiza.


Aidha, amewahimiza walimu na jamii nzima, kuwa walinzi wa miundombinu hiyo kwa kuitunza ili iweze kudumu kwa muda mrefu ikiwemo kuwasimamia wanafunzi kuzingatia suala la usafi kwa kutokuchora kuta za ndani na nje za vyumba vya madarasa hayo ili kuendelea kuwa muonekano mzuri kwa muda mrefu.


Hata hivyo walimu hao licha ya kuishukuru Serikali kwa kuwajengea vyumba hivyo vya madarasa, wameiomba serikali kuwajengea nyumba za walimu ili kuwawezesha kutekeleza majuku yao kwa urahisi kwani shule ipo mbali na maeneo ya makazi yao hali inayossababisha kuchelewa kuingia kwenye vipindi na kuzorotesha ufaulu wa wanafunzi.


“Tunaishukuru Serikali kwa kutujengea madarasa ambayo yatawapa fursa wanafunzi kujua kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK), kwa urahisi tofauti na ilivyokuwa hapo awali, wanafunzi walilazimika kupokezana kuingia darasani kutokana na uhaba wa madarasa, lakini sasa tunaamini ufaulu utaongezeka” Amesema mwl. Ratibu Shekaratha.


Aidha, Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Neema Hekarat ameahidi kusimamia suala usafi kwenye miundominu hiyo pamoja kusimamia kupandisha kiwango cha ufaulu wa wanafunzi hasa kupitia miihani mbali mbali ya kujipima na kuvuka kwenye asilimia 31.2 ambazo shule hiyo imepata,  kwenye matokeo ya upimaji wa mtihani Taifa wa kujipima wa darasa la saba mwaka 2023.


Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa