Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K Mongella ameuagiza uongozi wa Jiji la Arusha kukamilisha mradi wa ujenzi na ununuzi wa samani za shule mpya ya msingi Msasani B kata ya Muriet, Jiji la Arusha.
Mkuu huyo wa mkoa, ametoa agizo hilo mara baada ya kutembelea mradi huo na kujionea maendeleo ya ujenzi wa miundombinu, unaotekelezwa na serikali kwa gharama ya shilingi milioni 543, kupitia programu ya kuboresha upatikanaji wa fursa sawa katika ujifunzaji bora kwa Elimu ya awalinna msingi Tanzania Bara (SEQUIP).
Amesema kuwa licha ya majengo yote ya shule hiyo kukamilika, ametoa siku saba kukamilisha manunuzi ya samani zote na kuziweka shuleni hapo, ikiwemo madawati ya wanafunzi wa shule ya msingi, viti na meza pamoja na vifaa vya kuchezea kwa wanafunzi wa darasa la awali.
"Ninatoa siku saba, kuhakikisha samani zote za shule zinawekwa kwenye madarasa na ofiisi kwa kuwa ni sehemu ya maelekezo ya mradi mzima, hakikisheni Alhamisi ijayo kila kitu kipo hapa shuleni, nitakuja kukagua na ninatarajia kukuta kila kitu kimekamilika" Ameweka wazi Mkuu wa mkoa Mongella.
Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Jiji la Arusha Mhandisi Juma Hamsini
amemshukuru mkuu wa mkoa kwa kutembelea mradi huo na kuahidi kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi ili kukamilisha mahitaji yote ya mradi huo.
Amesema kuwa, ingawa mradi huu umekamilika katika ujenzi wa miundombinu lakini imebaki kuweka samani za madarasa na ofisi pamoja na vifaa vya michezo kwa wanafunzi wa darasa la awali.
Naye mwenyekiti wa mtaa wa Msasani Mhe. Rashid Chidi amemshukuru Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuwajengea shule nzuri katika mtaa wao, na zaidi ameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa miradi mingi ya maendeleo ambayo inawahudumia wananchi wa hali ya chini.
"Kata yetu ya Murieti ina watu wengi na watoto wengi sana, serikali inatujali sana, mara ya kwanza ilijenga shule nzuri ya Msasani kama mnavyoiona na sasa imetujengea shule nyingine nzuri Msasani B madarasa yanang'aa kama hoteli, serikali imetimiza jukumu lake sasa kazi iliyobaki na sisi wazazi kuwaleta watoto shuleni kusoma" Ameweka wazi Mwenyekiti huyo
Naye Mwalimu msimamizi wa mradi huo na Mwalimu mkii wa shule mama ya Msasani, Mwl. Manale amesema kuwa shule ilipokea kiasi cha shilingi milioni 543 kwa ajili ya ujezni wa shule hiyo mpya uliojumuisha ujenzi wa vyumba 14 vya madara ya shule ya msini, ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa ya mafano ya awali, matundu 24 ya vyoo vya wanafunzi na walimu, jengo la utawala pamoja na samani za shule nzima.
ARUSHA FURSA LUKUKI
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa