- _Barabara ya Arusha - Longido - Namanga; ujenzi umegharamu Bilioni 4.6_
Mkuu wa Mkoa wa Arusha CPA Amos Gabriel Makalla @amosmakalla Alhamisi ya leo Septemba 05,2025, ameagiza kukamilka kwa mradi wa daraja la Tanganyeti lenye urefu wa Mita 40 kwenye barabara ya Arusha - Longido - Namanga kuelekea nchi jirani ya Kenya, mradi unatekelezwa na Serikali kwa gharama ya shilingi Bilioni 4.6 kupitia Wakala wa Barabara Tanzania - TANROADS na Mkandarasi wa Kampuni ya Jiangx Geo Engineering.
CPA Makalla ametoa agizo hilo, wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za utekelezaji wa miradi ya maendeleo wilaya ya Longido na kuwahimiza Mkandarasi wa mradi huo kuongeza kasi na kuhakikisha ujenzi huo muhimu kwa wananchi, unakamilika mwezi Desemba,2025 ili uanze kutoa huduma kwa wananchi.
"Ninamshukuru Mhe.Rais Dkt. @samia_suluhu_hassan kwa kuona umuhimu wa ujenzi wa daraja kwenye barabara hii ambao ni muhimu kwa uchumi wa nchi hizi mbili za Tanzani na Kenya, hivyo kwa kuzingatia umuhimu wake, ujenzi uendane na kasi ya uhitaji wa huduma kwa wananchi pamoja na wageni wanaotumia barabara hii"Amesema
Hata hivyo wazee wa wilaya ya Longido wameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za kujenga daraja hilo kwenye eneo ambalo msimu wa mvua hujaa maji na kusababisha kero kubwa kwa watumiaji wa barabara hiyo.
Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Mkoa wa Arusha Mzee Michael Lekule Laizer, amebainisha, licha ya Mhe.Rais kutoa shilingi Bilioni 4.6 za kujenga daraja hilo, lakini ametoa fedha nyingi zilizotekelza miradi mikubwa ya afya,elimi laji na mindombinu ya barabara.
Awali aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Longido, ambaye ni Naibu Waziri wa Madini, Dkt Steven Kiruswa amemshukuru Rais Dkt. Samia kwa miradi mingi ya maendeleo iliyotekelezwa Wilayani humo katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake na kumuhakikishia kuwa, wananchi wa Longido wanaimani kubwa naye.
@longido.district_council @ortamisemi @tanroadshq @monduli_dc
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa