Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.CPA Amos Gabriel Makalla @amosmakalla amekutana na kufanya mazungumzo na Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma Mkoa wa Arusha, Mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano Ofisini ya Mkuu wa Mkoa mchana wa leo Agosti 29,2025.
Katika kikao kazi hicho chenye lengo la kufahamiana, CPA Makalla amewasisitiza Wakuu hao, umuhimu wa kushirikiana katika kutimiza majukumu yao ya kuwatumikia wananchi, ambayo ndio matarajio na malengo ya Serikali katika mkoa wa Arusha.
"Kama Viongozi wa Taasisi za Umma lazima tufanye kazi kwa bidii ili wananchi wapate huduma stahiki pamoja na kutambua umuhimu wa Taasisi hizo katika maeneo yao.
Aidha ameziagiza Taasisi zinatoa huduma za msingi za jamii ikiwemo maji, umeme na miundombinu ya barabara, kujipanga kikamilifu kukamilisha ujenzi wa miundombinu kwenywe eneo linalojengwa uwanja wa Mpira wa miguu ikiwa ni maandalizi ya mashindano ya mpira wa miguu barani Afrika, AFCON 2027.
Hata hivyo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Bwana Missaile Albano Musa, kwa niaba ya wakuu hao wa Taasisi, amemkaribisha CPA. Makalla na kumuahidi ushirikiano katika kuwatumikia wananchi huku akiahidi kusimamia kwa karibu utekelzaji wa miradi ya kutoa huduma muhimu za kijamii katika eneo unapojengwa uwanja utakaotumika kwenye michuano ya AFCON 2027.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa