_Kuwasomea Wananchi Taarifa ya Mapato na Matumizi sio Hisani; ni Wajibu_
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe.CPA Amos Gabriel Makalla Amos Makalla makalla amewagiza Watendaji na Wenyeviti wa Vijiji na vitongoji, kufanya mikutano ya kisheria kila baada ya miezi mitatu ili kusoma Taarifa ya Mapato na Matumizi kwa kuwa, kuwasomea wananchi Taarifa ya Mapato na matumizi ya kijiji sio hisani bali ni wajibu wa viongozi hao.
CPA Makalla ametoa rai hiyo wakati akizungumza na viongozi wa wananchi, Chama, mila pamoja na watalamu wa halmashauri ya wilaya ya Longido, Mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano halmashauri ya Longido Septemba 04, 2025.
Amewasisitiza viongozi hao, kuwa wanayodhamana kubwa waliyopewa na Serikali ya kuwatumikia na kuwahudumia wananchi na kutokusoma taarifa ya mapato na matumizi ya vijiji inawafanya wananchi kutokufahamu taarifa sahihi za maendeleo ya kijiji chao, jambo ambalo linaleta migogoro mingi na kuwafanya kuichukia Serikali yao.
Aidha, amewataka viongozi hao kuwahakikshia wananchi suala la amani na utulivu kayika maeneo yao kwa kuwasaidia kutatua migogoro miongoni mwao bila kufikshana mahakamani, kwa kuwa wananchi wengi wanakosa haki zao kwa kushindwa kumudu gharama kubwa za kuendesha kesi.
"Niwasihi viongozi wa ngazi zote, tumieni dhamana mliyopewa na Serikali, kuwahudumia wananchi, tatueni kero na migogoro kwa njia ya amani, kwa kufanya hivyo wananchi watajielekeza kwenye shughuli za maendleeo badala ya kupoteza muda kwenye kutafuta haki"
Hata hivyo, amewataka wananchi wote wa Longido kuhakikisha wanatumia haki yao ya kikatiba ya kupiga kura kwa kushiriki Uchaguzi Mkuu Oktoba, 29 na kuwasisitiza kwenye mikutano ya Kampeni ili kusikiliza sera za vyama vya Siasa, sera ambazo zitawasukuma kufanya maamuzi sahihi wakati wa kupiga kura kwa kuchagua viongozi wenye mapenzi mema na nchi yao.
#kaziinaendelea
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa