Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amewataka watanzania kufanya tafiti ikiwa walioondolewa kwenye baraza la Mawaziri kwenye serikali ya awamu ya sita, ikiwa wanahusika na madai aliyoyatoa wakati wa kumbukizi ya miaka 40 ya kifo cha Hayati Edward Moringe Sokoine, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania.
Mhe. Makonda ametoa kauli hiyo leo Jumapili Novemba 17, 2024 wakati Mkuu wa Mkoa alipokuwa akijibu maswali kutoka kwa wanahabari wanaoshiriki kwenye Hafla ya kutoa tathimini ya miezi sita ya Uongozi wake kama Mkuu wa Mkoa wa Arusha tangu kuteuliwa kwake Aprili 08, 2024.
Katika maswali hayo, Mhe. Makonda aliulizwa kuhusu kauli yake ya kutaka kuwataja watanzania na baadhi ya Mawaziri ambao wamekuwa wakimtusi na kumkashifu Rais Samia Suluhu Hassan ambapo Mhe. Makonda alikiri kuwa aliwasiliana na Mhe. Rais Samia kama alivyoahidi na suala hilo limebakia kuwa siri kati yake ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa