• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

RC MAKONDA AMSHUKURU DKT. SAMIA KWA KUIJALI ARUSHA; AZINDUA MAGARI MAWILI YA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI ARUSHA

Posted on: May 22nd, 2024

Na Elinipa Lupembe

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda, amemshukuru na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuujali mkoa wa Arusha huku akiungalia kwa jicho la kipekee, na kuwezesha miradi mingi ya maendeleo mkoani humo, kutoka na malengo ya kuimarisha sekta ya Utilii, sekta inayoingiza fedha nyingi za kigeni nchini.

Mhe. Makonda, ametoa shukurani hizo, wakati akizindua magari mawili na kukabidhi kwa kikosi cha Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Arusha, hafla iliyofanyika kwenye Ofisi kuu za Jeshi hilo, mapema leo Mei 20, 2024.

Amebainisha kuwa, Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt. Samia, inafanya kazi kubwa ya kupeleka maendeleo karibu na wananchi kona zote nchini huku mkoa wa Arusha ukinufaika zaidi katika sekta zote ikiwemo kuimarisha zaidi, eneo la ulinzi na usalama wa mkoa huo.

Mhe. Makonda amekiri kuwa, katika kuimarisha usalama  wa mkoa wa Arusha, Mhe. Rais ametoa magari 2 kati ya magari 12 yaliyogawiwa nchi nzima,  magari ambayo ni mapya na ya kisasa ili kuwezesha utendaji kazi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,  yanakwenda kuimarisha usalama wananachi na mali zao katika mkoa huo.

"Tumepewa magari mawili kwa Jeshi letu la Zimamoto na Uokoaji na kufanya mkoa kuwa na magari 6 sasa, kila mmoja ni shahidi wa jitihada kubwa za  Dkt.Samia za kuhakikisha mkoa wa Arusha unakua katika sekta zote, kwa miaka mitatu ametoa takribani trilioni 1.8 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo kisekta lakini zaidi anawekeza nguvu kubwa katika kuimarisha sekta ya Utalii kwa lengo la kukuza uchumi wa mkoa wa Arusha na Taifa la Tanzania" Amesema  Mhe. Makonda

Hata hivyo, ameweka wazi kuwa, kwa kuwa asilimia 80 ya Uchumi wa mkoa  huo, unategemea wageni wa ndani na nje ya nchi ambao wanafika kwa ajili ya shuguli za kikazi na zaidi utalii, shughuli ambazo zinahitaji usalama wa uhakika wa watu na mali zao.

Awali, Mhe. Makonda amezindua magari hayo ya kisasa yaliyotolewa na Serikali ya awamu ya sita, kwa ajili ya shughuli za kuzima moto na ukoaji, yenye thamani ya takribani shilingi bilioni 1.9.

Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa