• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

RC MAKONDA ATAKA BODA YA NAMANGA KUTUMIA TEKNOLOJIA ZA KISASA KATIKA UTENDAJI..

Posted on: April 19th, 2024

Na Elinipa Lupembe

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Paul Christian Makonda, amewataka watumishi wa Kituo cha Huduma ya Pamoja Namanga kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya, kutumia technolojia za kisasa katika utendaji kazi ili kuharakisha utoaji wa huduma kwa wasafiri.

Mhe. Makonda amesema hayo alipotembelea Kituoni hapo na kutoridhishwa na utoaji wa huduma katika kituo ambacho ni muhimu kwa maingiliano na huduma ya usafiri na usafirishaji kati ya mataifa mawili ya Tanzania na Kenya yenye kuhusiana kibiashara na kijamii kwa muda mrefu hivi sasa.

Aidha, amebainisha kuwa huduma katika kituo hicho zinacheleweshwa na kuchukua muda mrefu kutokana na kutotumia teknolojia kikamilifu hasa katika ukaguzi wa Wageni na uidhinishaji wa mizigo, unaofanywa na taasisi za Serikali zilizopo kituoni hapo.

"Kituo cha Namanga kinatakiwa  kuwa Kituo namba moja kati ya vituo vyte vya  mipakani katika utoaji wa huduma bora kwa wageni na wasafiri, Ili kuongeza wigo wa mizigo na wageni wengi zaidi kuingia mkoani Arusha na hivyo kuchochea uchumi wa Arusha na Tanzania kwa ujumla wake" . Ameweka wazi Mhe Makonda

Ameongeza kuwa, suala  ni muhimu katika kutekeleza maagizo ya Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya ukuzaji wa Utalii katika mkoa wa Arusha, ambapo anahimiza utoaji na upatikanaji wa huduma bora na rafiki kwa wateja Katika suala la matumizi ya teknolojia.

Ameutaka Uongozi wa Kituo cha pamoja Namanga kuwaunganisha wateja wao na mitandao ya simu ili wanapoingia nchini wawe na uwezo wa kuanza kutumia laini za simu kwa mitandao ya simu iliyopo nchini kwa kusajiliwa kupitia nyaraka wanazoziwasilisha kituoni hapo.

Awali, amewahimiza watumishi wa kituo hicho, kuwa mabalozi wazuri wa Utalii kwa kutoa huduma bora kwa wageni kwa kuwaeleza mazuri ya Tanzania pamoja na vivutio vya utalii vinavyopatikana Arusha ili kushiriki kikamilifu katika kuukuza Utalii na uchumi wa Tanzania.


Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa