• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

RC MAKONDA AZUNGUMZA  NA WATUMISHI WA WILAYA YA LONGIDO; ASISITIZA KIPAUMBELE CHAKE NI KAZI

Posted on: May 23rd, 2024

Na Elinipa Lupembe

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda, amewasili wilaya ya Longido na kupokelewa na Mkuu wa wilaya hiyo Mhe. Marco Ng'umbi ofisini kwake mapema leo Mei 23, 2024 na kuwataka viongozi na watumushi kuwajibika na kutambua kuwa kipaumbele chake ni kazi.

Mhe. Makonda yuko wilayani Longido, ikiwa ni zara yake ya kwanza ya kikazi ya kutembelea wilaya za mkoa wa Arusha, na kukutana na viongozi wa Chama, Serikali, Jamii na Watumishi wa Wilaya hiyo na kuweka wazi kuwa, amefika wilayani humo licha ya kufanya shughuli za kikazi ni fursa yake ya kipekee ya kufahamiana pamoja na kuangalia namna ya utendaji kazi wa viongozi na watumishi katika kuhudumia wananchi.

Amewataka viongozi na  watumishi wote kutambua dhamana kubwa waliyoibeba ya kuwahudumia wananchi na kutojishahau, badala yake kuheshimu dhamana hiyo kwa kufanya kazi huku wakitambua kipaumbele chao pekee  ni kazi na si vinginevyo.

" Viongozi na Watumishi wetu wafahamu, kila mmoja kwa nafasi yake anapaswa kutambua wananchi ndio 'maboss'  wetu ambao wametuajiri na kutuweka madarakarakani, hivyo ni vema kila mtu kutekeleza majukumu yake na kuhakikisha wananchi wanahudumiwa ipasavyo" Amebainisha Mhe.Makonda

Hata hivyo, ameweka wazi matamanio yake ni kuona  wananchi wanatambusa kuwa, Serikali ya awamu ya sita chini ya Jemadari Dkt. Samia Suluhu Hassan inawathamini sana hivyo, watumishi waliopewa dhamana yananalo jukumu la kutimiza wajibu wao ndio heshima ya utumishi wa Umma.

"Mwananchi anatakiwa kujisikia fahari kuhudumiwa na Serikali yake pendwa, huku akitambua huduma za kijamii zilizoletwa na Serikali kwenye eneo lake ni kazi kubwa ya Dkt.Samia"

Amewakumbusha Waheshimiwa Madiwani kupitia Baraza lao, wanayo dhamana kubwa kwa kuwa wao ni wawakilishi wa wananchi hivyo jukumu lao ni kuhakikisha, wanashughulikia kero za wananchi kwa kuzibeba na kuziwasilisha kwenye vikao halali vya halmashauri ili ziweze kutafutiwa ufumbuzi.

"Dhamana ya uongozi mliyopewa ni kuwahudumia wananchi"

Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa