Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Christian Makonda atakuwa mwenyeji wa Kongamano la Uwekezaji katika Sekta ya Utalii nchini, linatofanyia tarehe 30 Mei, 2024 kwenye Ukumbi wa Gran Melia Jijini Arusha.
Mkutano huo utaongozwa na Waziri wa Nchi, ofisi ya Rais, mipango na uwekezaji Mhe. Profesa Kitila Mkumbo kwa kushirikiana na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Angela Kairuki.
Kongamano hilo linafuatia maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan alilolitoa wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali akimtaka Mkuu wa Mkoa wa Arusha kushughulikia changamoto ya upatikanaji wa vyumba vya kulala wageni wanaotembelea Mkoa wa Arusha.
Kongamano hilo litajumuisha Viongozi wa serikali na wadau mbalimbali katika sekta ya Utalii nchini Tanzania kwa lengo la kuona namna ya Kukuza uwekezaji katika sekta hiyo hususani kwa kuongeza ujazo wa vitanda kwaajili ya kuwatosheleza wageni mbalimbali.
Kauli Mbiu: Uwekezaji Katika Utalii Endelevu, Uchangamkiaji wa fursa za Uwekezaji baada ya Program ya Tanzania 'The Royal Tour'.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa