• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

RC MONGELLA AAGIZA LORI  LA KLINIKI TEMBEZI KUANZA KAZI NGORONGORO...

Posted on: December 5th, 2023

Na Elinipa Lupembe


Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K.Mongella amemkabidhi Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Dkt. Charles Rashid Mkombachepa, Lori la Kliniki Tembezi (mobile clinic) na kuagiza kuanza, mara moja, kufanya kazi kwenye halmashauri ya Ngorongoro.


Mhe. Mongella ameweka wazi kuwa,  Lori hilo la Kilini tembezi, limeletwa kufuatia mkakati wa uboreshaji na uimarishaji wa huduma za Afya, hususani huduma za dharura na kuongeza kuwa, mkoa unaanza rasmi utekelezaji huo, kwa kuelekeza Lori hilo kutumiwa na Madaktari Bingwa, kutoa huduma kwa wagonjwa walio kwenye maeneo ya pembezoni, ambayo hayafikiki kwa wepesi.


Mhe. Mongella, hakusita kumshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwajali wananchi wa Arusha, ambao Jiografia ya maeneo mengi ni magumu na hayafikiki kwa wepesi na watu wake wanaishi kwa mtawanyiko mkubwa, ambao wanahitaji huduma za afya kuwafikia kwa karibu.


Aidha, Mhe. Mongella amemsisitiza Mganga Mkuu wa mkoa, kuhakikisha anawapangia Madaktari Bingwa, kwenye halmashauri za pembezoni kwa kuanza na wilaya ya Ngorongoro, Longido na baadhi ya maeneo ya Arumeru, ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma ndani ya maeneo yao, kama yalivyo malengo ya Serikali.


"Mama Samia ameshafanya kazi yake, kaai iliyopaki ni sisi kumsaidia kuhakikisha wananchi wanapata huduma, ninakuagiza Mganga Mkuu, gari hili likafanye kazi iliyokusudiwa ya kuwahudumia wagonjwa kwenye maeneo yao, madaktari wapangiwe na kuanza kazi kwenye wilaya ya Ngorongoro na madaktari walifuate gari hilo na kutoa huduma kwa wananchi, kwenye maeneo yao" Amesisistiza


Awali, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Dkt. Mkombachepa, amesema kuwa, wamepokea magari manne yenye thamani ya shilingi milioni 646.3, kutoka Serikali kupitia Ofisi ya Rais - TAMISEMI, ikiwa ni mkakati wa Serikali wa  uboreshaji na uimarishaji wa huduma za afya hususani huduma za dharura na rufaa pamoja na kusogeza huduma zaidi karibu na wananchi.


Amefafanua kuwa,  magari hayo manne aina ya Toyota Land Cruiser Ambulance 3, zimegawiwa kwenye wilaya ya Ngorongoro, Longido na Hospitali ya Rufaa mkoa wa Arusha, huku Lori la Kliniki Tembezi likikabidhiwa Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa kwa ajli ya kufanya kazi za kutoa huduma kuzunguka mkoa mzima.


Hata hivyo, Dkt. Mkombapepa kwa niaba ya watumishi wa Afya, ameishukuru Serikali ya awamu ya sita, kwa kuwa na mkakati wa kutoa vitendea kazi kwenye Idara ya afya, vieteneakazi ambavyo vinakwenda kuwarahisishia kazi wahudumu hao, huku akiahidia kusimamia utunzania na matumizi sahihi ya vifaa pamoja na kuhakikisha wananchi wanapata huduma stahiki.


#ArushaFursaLukuki


Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa