• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

RC MONGELLA AAGIZA VITUO VYOTE VYA AFYA KUTUMIA MFUMO GotHoMIS..

Posted on: October 24th, 2023

Na Elinipa Lupembe


Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. John V.K. Mongella amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote za mkoa wa Arusha kuhakikisha vituo vyote vya kutolea huduma za Afya vinafungwa mfumo wa kumeneji taarifa na kukusanyia Mapato wa GoT HoMIS, mfumo ambao licha ya kuthibiti ukusanyaji wa Mapato unasaidia kutunza kumbukumbu za matibabu ya wagonjwa, wanaofika kituoni kuapta huduma za afya.


Mkuu huyo wa mkoa ametoa agizo hilo wakati akikagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Karatu na kujionea namna mfumo huo wa GoT HoMIS unavyofanya kazi na kusisitiza kuwa kila kituo cha Afya kinalazimika kufungwa na kutumia mfumo huo kama yalivyo maagizo na maelekezo ya Serikali.


Amesema kuwa Serikali imeandaa mfumo huo muhimu kwa lengo la kumeneji huduma zinazotolewa na hospitali kwa wagonjwa pamoja na kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato na dawa zinazoingia na kutolewa kwa wagonjwa.


Ameweka wazi kuwa licha ya mahitaji mengi ya Halmashauri,  Halmashauri zinatakiwa kuweka kipaumbele kwenye bajeti zao kwa ajili ya kufunga mifumo hiyo ili kuboresha utoaji na upatikanaji wa huduma za afya zenye ubora kwa wananchi ambalo ndilo lengo kuu la Serikali ya awamu ya sita la kujenga vituo hivyo karibu na maeneo ya wananchi.


"Kupitia mfumo huo tutapata takwimu sahihi za wagonjwa, wanaohudumiwa kwa siku, matibabu waliyopatiwa, dawa walizotumia pamoja na kiasi cha fedha kilichokusanywa, Mfumo huu ni muhimu sana licha ya kuwa wapo wahudumu wasiopenda kuutumia, ifike mahali tuhame kwenye mifumo ya analojia tuingie kwenye utoaji huduma wa Kidigitali kwa kuwa unaokoa muda pia" Ameweka wazi Mhe. Mongella


Awali Mkuu huyo wa Mkoa ametembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Hospitali hiyo ya wilaya mradi unatekelezwa na Serikali kwa gharama ya zaidi ya Bilioni 3.5 lengo likiwa ni kusogeza utoaji na upatikanaji wa huduma za afya karibu na wanachi


Ikumbukwe kuwa, ujenzi wa Hospitali za wilaya ni Utekelzaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM, Ibara ya 81 Ujenzi na Ukarabati wa Vituo vya Kutolea Huduma ya Afya ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Hospitali za Wilaya nchini


#ArushaFursaLukuki

Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa