• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

RC MONGELLA AKABIDHI MSAADA WA CHAKULA KWA WATOTO YATIMA WA MAKAZI YA THE JOY OF GOD

Posted on: February 3rd, 2024


Na Elinipa Lupembe 


Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K Mongella, ametoa msaada wa vyakula kwa watoto yatima, kwenye makazi ya 'The Joy of God Ophanance' ya Jijini Arusha, kupitia fedha walizozawadiwa na watumishi wa Sekretariet mkoa wa Arusha, wakati wa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa 2024.


Mhe. Mongella ametimiza ahadi yake Februari 02, 2024, aliyoitoa siku ya sherehe  ya kukaribisha mwaka 2024, baada ya watumishi wa Sekretariet mkoa wa Arusha, kuwazawadia fedha yeye na Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Missaile Albano Musa pamoja na Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu, David Francis Lyamongi, na kuahidi fedha hizo kuzipeleka kwa watoto yatima.


"Tunawashukuru watumishi wote kwa zawadi hii mliyotupatia, tunaithamini sana na kutambua umuhimu wake, lakini fedha hizi tutanunua chakula na kupeleka kwa watoto yatima, Sista wa kituo cha The Joy of God, amenipigia simu kuwa wana uhitaji wa chakula katika kituo hicho" Aliahidi Mhe. Mongella.


Akizungumza mara baada ya kupokea chakula hicho, Msimamizi wa kituo hicho, Sista. Janeth Mosten Ngopa,  licha ya kumshukuru sana Mhe. Mongella kwa upendo na huruma yake ya kuwakumbuka na kuwajali watoto yatima, na kusema kuwa, zawadi ya chakula kwa watoto hao ina thamani kuwa, kwa kuwa uwepo wa chakula cha kutosha kituoni, unawakikishia afya watoto hawa pamoja na kuwafanya kuwa na furaha na matumaini kwakati wote.


“Tunamshukuru sana Mhe. Mongella kwa upendo wake kwetu na moyo wake wa kutoa, tunamuombea kwa Mungu azidi kumbariki, kupitia yeye watoto hawa wanafarajika, hata sisi walezi tunakuwa na amani, zaidi sana tunamshuru Mhe. Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan, kwa kutuletea Mhe. Mongella Arusha, kiongozi mwenye upendo wa dhati kwa wananchi wake bila kujali hali zao, amekuwa ni sehemu ya familia katika vituo vya kulelea watoto yatima na wenye uhitaji, hatujawahi kuomba msaada kwake tukakosa, Mungu akubariki sana ”. Amesema Sister Ngopa


Hata hivyo, watoto hao wamemshukuru Mkuu huyo wa Mkoa, kwa kuwajali na kujitoa mara zote bila kuchoka, kwa kuwa amekuwa akiwatembelea mara kwa mara na kuwapa mahitaji tofauti tofauti na kuahidi kuendelea kumuombea baraka kutoka kwa Mungu.


“Kupitia chakula hiki tunamuombea sana mkuu wa mkoa, Mungu ampe maisha marefu na azidi kumbariki kwa kumzidishia  mara dufu pale alipotoa kwaajili yetu”. Amesema Dominick Denis.


Awali, vyakula vilivokabidhiwa ni pamoja na Kg 150 za Mchele Kg 65 za unga wa mahindi, Kg 100 na Kg 50 za maharage  vyote vikiwa na thamani ya shilingi 822,000.


#arushafursalukuki



Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa