• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

RC MONGELLA AKAGUA JENGO LA WAGONJWA WA NJE (OPD COMPLEX) HOSPITALI YA JIJI LA ARUSHA.

Posted on: October 18th, 2023

Na Elinipa Lupembe.

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. John V.K. Mongella, ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Jengo la wagonjwa wa Nje OPD Complex  hospitali ya Jiji la  Arusha mradi unaotekelezwa kwa gharama ya shilingi bilioni 1.6 kwa lengo la kusogeza huduma za afya karibu na wananchi.

Mradi huo ni unatekelezwa kwa fedha kutoka serikali kuu shilingi bilioni 1 ikiwa ni ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani wakati alipozindua hospitali hiyo mwaka 2021 na kutoa ahadi ambayo tayari serikali imezitoa na milioni 655 fedha za mapato ya ndani ya Jiji.

Hata hivyo Mhe. Mongella ameshukuru mheshimia Rais mama Samia kwa kuwajali na kuwathamini wananchi wa Arusha kwa kuwa hospitali hiyo ni muhimu kwa utoaji na upatikanaji wa huduma za afya na kuongeza kuwa licha ya kuwahudumia wananchi wa Jiji la Arusha lakini ni mkakati wa kupunguza msongamao wa wagonjwa kwenye hospitali ya Rufaa ya Mount Meru.

Aidha amesema kuwa serilikali chini ya usimamizi wa mheshimiwa Rais, ameshatekeleza ahadi yake, kazi iliyobaki ni Jiji la Arusha kuendelea kutumia mapato yake ya ndani kukamilisha jengo hilo ili liweze kutoa huduma kwa wananchi ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020 kuelekea 2025.

"Serikali katika kutekeeleza Ilani ya CCM  mkoa wa Arusha, serikali imefanikiwa kujenga hospitali katika  wilaya ya Karatu, Longido, Monduli na sasa inakamilisha hospitali hii ya wilaya ya Arusha pamoja na zahanati na vituo vya afya vya kutosha katika halmashauri zote za mkoa wa Arusha" Ameweka wazi Mhe. Mongella

Amewataka watalamu wasimamizi wa mradi huo kuhakikisha mradi huo, unakamilika kwa wakati ukiwa na viwango vinavyoendana na thamani ya fedha zinazotolewa na serikali.

Awali awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mradi huo wenye gharama ya Bilioni 1.6 utahusisha ujenzi wa sakafu ya chini ya jengo hilo, likibena ofisi za Idara ya dharura, idara ya mionzi, Idara ya ushauri wa kidaktari na usafishaji damu, pamoja na Huduma za uchunguzi wa mwili mzima.

 #ArushaFursaLukuki
#KaziInaendelea


Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa