• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

RC MONGELLA AMUELEZEA MAREHEMU ZELOTHE ; ALIKUWA KIONGOZI ALIYENYOOKA....

Posted on: October 28th, 2023

Na Elinipa Lupembe


Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. John V.K Mongella amemuelezea Marehemu Zelothe Stephene Zelothe aliyekuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi (mstaafu) wa Jeshi la polisi nchini na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha, kuwa alikuwa ni Kiongozi aliyenyooka na mwenye msimamo kwa mambo ya msingi, muadilifu, mzalendo na mwenye kupenda watu na mwenye bidii katika kazi.


Mhe Mongella ameeleza hayo mara baada ya sala fupi iliyofanyika nje ya jengo la kuhifadhia maiti,  Hosptali ya Rufaa ya mkoa wa Arusha, muda mfupi baada ya kuwasili mkoani Arusha na kuhifadhi mwili huo hospitalini hapo.


Ameanza kwa kumshukuru Mwenyenzi Mungu kwa fursa aliyoitoa kwa maisha ya Mzee Zelothe hapa duniani, na kukiri kwamba kila mwanandamu anayosafari yake na mwisho huwa ni kifo na kusema kuwa marehemu Zelothe alikuwa ni Kiongozi hodari mwenye hekima nyingi na kauli thabiti, aliyenyooka na asiyekurupuka katika kufanya maamuzi.


Amethibitisha kuwa, katika kipindi chote ambacho mzee  Zelothe amefanya kazi, akilitumikia Jeshi la Polisi kwa nafasi mbalimbali, akiwa Mkuu wa wilaya ya Musoma, mkuu wa mkoa Rukwa na baadaye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa mkoa wa Arusha (NEC), amekuwa ni kiongozi mwenye nidhamu, mwadilifu, mwenye hekima, zaidi mwenye kupenda watu na kufanya kazi kwa bidii.


"Nachelea kusema Marehemu alikuwa ni mtu 'smart', amenyooka, asiye penda konakona, alipenda  kufanya kazi kwa kushirikiana na wengine, aliwaunganisha watu na kuwa kitu kimoja, aliamini kwenye falsafa ya ushirikishwaji, alikuwa ni kiongozi na mwalimu wa kila mtu, sisi wengine tumejifunza mengi kutoka kwake" Amesema


Aidha amekiri kuwa ingawa pengo la mzee Zelothe halitazibika lakini ameahidi kuyaenzi maisha yake, na kuendeleza yale yote mema aliyoyafanya akiwa mtumishi wa Umma, kama baba, kama kiongozi na zaidi kama mwanachama muadilifu wa Chama Cha Mapinduzi.


Awali, Mrehemu Zelothe alifariki tarehe 26.10.2023 Jijini Dare es salaam akiwa napatiwa matibabu na mwili wake kuwasili Arusha 28.10.2023 huku mazishi yakitarajiwa kufanyika siku ya Jumatatu 30.10.2023 nyumbani kwake kitongoji cha Olosiva kata ya Oloirieni wilaya ya Arumeru.


Bwana Ametoa, Bwana Ametwaa, Jina lake Lihimidiwe

Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa