• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

RC MONGELLA ATATUA MGOGORO WA KIWANJA NJIRO; AAGIZA KAMISHNA KUTAO HATI NDANI YA SIKU SABA.

Posted on: March 15th, 2024


Na Elinipa Lupembe 


Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K.Mongella, ametatua mgogoro wa Kiwanja namba 624 na 625 Block F eneo la Njiro, Jijini Arusha, mgogoro uliodumu zaidi ya miaka 17, na kuwataka Maafisa Ardhi kuandaa hati ndani ya siku 7. 


Mhe. Mongella ametatua mgogoro huo, mara baada ya kuzungumza na kwenda eneo la kiwanja na walalamikaji Anansia Everest na mwenzake waliowalalamikia Maofisa wa Ardhi kumgawia eneo la kiwanja hicho mtu mwingine anayejulikana kwa jina la Jeina.


Baada ya mazungumzo ya kina, kutoka pande zote, Mhe. Mongella amewaagiza Kamishna wa Ardhi mkoa wa rusha, kutengeneza hati za watu wote watatu kwa kutumia 'title deed' iliyopo na kurekebisha ukubwa wa viwanja hivyo ili wote watatu wapate hati miliki mpya kila mmoja na eneo lake.


"Kwa kuwa 'title deed na code nates' zipo, ninawapa wiki moja kufanya hili zoezi, rekebisheni ukubwa wa eneo, andaeni hati nyingine, kila mmoja apate hati mpya, kiwanja kimoja kitakuwa na mita za mraba 588, cha pili 740 na wa tatu atabaki na mita za mraba 440 na kila mmoja anapopewa hati mpya arudishe ile hati ya awali" Amefafanua Mhe. Mongella


Hata hivyo, walalamikaji wote wameridhishwa na maamuzi hayo na kukubali kupatiwa hati mpya kwa mujibu wa maelekezo yaliyotolewa na Mkuu wa mkoa huyo kulingana na title deed iliyopo.


Naye mlalamikaji wa kwanza, Anasia Evarest Malewas, amemshukuru mkuu wa mkoa, kwa kufanya maamuzi yanye hekimq na busara ambayo yametuwezesha wote kuoata haki, na sio kupata haki bali kila mmoja kupata eneo, eneo ambalo tumelihangaikia kwa muda mferu.


"Binafsi ninamshukuru mkuu wa mkoa, Mungu ambariki sana,  ninaamini sote tutapata haki yetu, ambayo tumezunguka kuhangaika na eneo hili, kwa miaka 17 sasa, huyu baba Mungu ambarikia sana" Amesema Anansia


Lembris Kipuyo, ambaye ni mtetezi wa walalamikaji ambao amedzi yeye ni mtetezi na mwakilishi wa wajane, amemshuru pia mkuu wa mkoa kwa maamuzi mazuri yanayokwenda kuwapa haki kina mama hao wajane ambao walikuwa na hati na wakizilipia lakini viwanja vyao vilikuwa na mkanganyiko wa kiufundi.


Aidha, ametoa wito kwa Maofisa wa Ardhi, kutambua na kuthamini kazi wanayoifanya kwa kutenda haki kwa watanzania na sio kuwa vyanzo vya migogoro, migogoro haijengi bali inajeruhi mioyo ya watu na kusababisha chuki miongoni mwa wanajamii ni vyema kuiepuka


Hata hivyo, Kamishna wa Ardhi mkoa wa Arusha, Geophray Mwamsojo, ameahidi kusimamia zoezi hilo na kuhakikisha hati hizo zinapatikana ndani ya siku 7 kama yalivyo maagizo na maelekezo ya Mheshimiwa mkuu wa Mkoa.


"Hapa changamoto ilikuwa ni uelewa mdogo na makubalino baina ya wateja wetu, tunashukuru leo RC ameweka hili jambo sawa, wameelewa na wote wameridhika, tunakwenda kuwapa hati zao kama ilivyokusudiwa,,lengo ni kuhakikisha kila mmoja amepata hati yake" Amefafanua Kamishina huyo wa Ardhi.


Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa