Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. John V.K Mongella ametembelea Hospitali ya wilaya Ngorongoro na kukakua maendeleo ya hospitali hiyo pamoja dawa na vifaa tiba vilivyonunuliwa mara baada ya serikali kutoa fedha kiasi cha shilingi milioni 100.
Mhe. Mongella ameendelea kuwasisitiza Wahudumu wa afya kutunza miundombinu iliyojengwa, vifaa tiba pamoja na matumizi sahii ya dawa kwa kuhakikisha wagonjwa wanapata dawa zilizotolewa na Serikali na si vinginevyo.
Amesisitiza kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha kila mtanzania anapata huduma bora na sahihi za afya, hivyo dahamana ya kuwahudumia wananchi hao ipo mikononi mwa wahudumu wa afya, wanapaswa kuwatendea haki wagonjwa
"Serikali imetekeleza jukumu lake, kazi ya kutunza vifaa hivi, kutoa huduma bora kwa wagpnjwa ni yenu madaktari na wauguzi, hakuna mtu atakuja kulinda vifaa hivyi, ni kazi yenu, kuweni wazalendo, msaidieni Rais Samia kuwahudumia wananchi wa Ngorongoro, amejenga hospitali hii ili wananchi wake wasiteseke" Amesisitiza kwa hisia Mhe. Mongella.
Kufuatia mkakati wa serikali ya awamu ya sita ya kila wilaya kuwa na hospitali, mpango huo umetekeleza kwa wiliaya ya Ngorongoro kwa kujeng Hospitali ya wilaya kwa gharama ya shilingi bilioni 3.4 na kuwekeza vifaa tiba vya shilingi milioni 100.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa