Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John V.K.Mongella, amewakaribisha Wahandisi wote walioshirikia Mkutano wa 32 waTaasisi ya Wahandisi Tanzania (IET), mkoani Arusha, alopoapata nafasi ya kutoa salamu za mkoa, mkutano unaofanyika, kwenye Kituo cha Mikutano ya Kimataifa Arusha (AICC) Mkoani Arusha.
Mkuu huyo wa Mkoa ametumia fursa hiyo kwanz kuwashukuru waandaaji wa mkutano huo, kwa kuchagua mkoa wa Arusha, kufanyika mkutano huo, muhimu kwa maendeleo nchi ya Tanzania na kuwataka wajisikie wapo nyumbani wawapo Arusha.
Aidha amewaahidi kuwapa ushirikiano pindi unapohitajiaka huku akiwahakikishia usalama wao, muda wote wawapo Arusha na kuwataka kufurahia hali ya hewa nzuri ya mkoa wa Arusha, inayovutia kwa kila mgeni ajaye mkoani hapo.
"Kwa niaba ya viongozi na wananchi wa mkoa wa Arusha, ninawakaribisha wote Arusha, mkoa huu ni moja ya mikoa ambayo inavivutio vingi vya utalii, tumieni wasaa huu kutembelea vivutio hivyo" Amesema Mhe. Mongella.
Hata hivyo, ameweka wazi kuwa, Wakuu wa mikoa wanatambua kazi kubwa inayofanywa na Wahandisi, kwenye Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, kazi ambazo ndio nguzo za maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla.
"Miradi inayotekelezwa kwenye mikoa na Mamlaka zake, inafanywa na Wahandisi, sisi kama wakuu wa mikoa, kwa niaba ya wakuu wa mikoa wenzangu, muda wote huwa, tunajisifu kwa kujinasibisha na kazi zinazofanywa na wahandisi kwenye maeneo yetu" Mhe. Mongella
Awali, Mkutano huo umefunguliwa ma Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa (MB), kwa kufunga kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, wenye dhima ya Suluhu za Ubunifu katika Uhandisi kwa maendeleo endelevu.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa