Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. V.K. Mongella ameupongeza uongozi wa wilaya ya Longido, Kamati ya Ulinzi na Usalama, viongozi wa Chama na wawakilishi wa wananchi kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kutekeleza shughuli za serikali za kuwahudumia wananchi wilayani humo.
Akizungumza kwenye kikao kifupi cha ukaribisho, Mhe. Mongella licha ya kuwapongeza watalamu hao kwa kufanya kazi nzuri ya usimaamizi wa miradi ya maendeleo, amewasihi kuhakikisha wanayafikia malengo yaliyokusudiwa na Serikali ya kutoa huduma bora na stahikinkwa wananchi.
Amethibitisha kuwa kwa sasa wilaya ya Longido imepiga hatua katika utekelzaji wa shughuli za serikali , shughuli ambazo kwa kiasi kikubwa zimefanikiwa kufikia malengo ya serikali tofauti na hapo awali, ameongeza kuwa kwa sasa Longido imetu,ia na inakwenda na kasi ya Serikali ya awamu ya sita.
"Niwapongeze kwa kazi kubwa inayofanyika Longido kwa sasa, niwatake tusonge mbele, wanaLongido hawataki maelezo wanataka maendeleo, miradi yote inatakiwa kukamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyoelekezwa kulingana na thamani ya fedha zilizotolewa na Serikali" Amesema Mhe. Mongella
Ameongeza kuwa, Serikali imewapa jukumu kubwa viongozi na watalamu katika usimamizi wa miradi, tumieni dhamana hiyo kumuunga mkono Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika usimamizi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa wakati na inayozingatia vigezo na viwango vya ubora.
"Sote tu mashahidi Serikali ya awamu ya sita imetoa fedha nyingi za kutekeleza na kukamilisha miradi ya maendeleo nchini, tofauti na awamu zilizotangulia, tusimkatishe tamaa Mhe. Rais, hakikisheni wananchi wanapata huduma stahiki na kwa wakati" Amesisitiza Mhe. Mongella
Awali mkuu wa mkoa wa Arusha yuko wilaya ya Longido kwa ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa shughuli za utekelezaji wa miradi ya Maendeleo na kukutana na uongozi wa wilaya hiyo.
#ArushaFursaLukuki
#KaziInaendelea
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa