• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

RC MONGELLA; WANANCHI WANALOHITAJI KUBWA LA KUELIMISHWA UMUHIMU WA KUFAHAMU HAKI ZAO NA NAMNA YA KUZIPATA

Posted on: February 1st, 2024


Na Elinipa Lupembe.


Taasisi zinazojishughulisha na Haki Jinai, zimeshauriwa kuwaelemisha wananchi  kufahamu umuhimu wa kuzitambua haki zao na namna bora ya kuzipata haki hizo, ili kuondokana na migogoro isiyokuwa ya lazima inayosababisha ukosefu na uvunjifu wa amani.


Rai hiyo, imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K Mongella, wakati alipopata fursa ya kuzungumza na hadhira iliyohudhuria sherehe za Kilele cha siku ya Sheria Nchini (Law Day) mwaka 2024,  ziliyofanyanyika kwenye viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, ameweka wazi kuwa hitaji kubwa la watanzania ni kufahamu haki zao na namna bora ya kuzipata.


Mhe. Mongella ameweka wazi kuwa, ili kupatikana kwa haki, mwananchi mwenyewe ana nafasi kubwa zaidi ya kujitafutia kwanza taarifa muhimu kuhusu haki zake, taarifa ambazo Taasisi hizo zinapaswa kuwawezesha kuzipata kupitia elimu zinazotolewa na kuwawezesha kuzisoma kwenye Tovuti za Taasisi za Umma.


Ameweka wazi kuwa, ili kuwarahisishia wananchi, kutambua namna bora ya upatikanaji wa Haki, amezishauri Taasisi zote  zinazohusika na Haki Jinai kuboresha mfumo

wa kazi zao, kwa kuziunganisha kupitia mifumo ya TEHAMA, kama inavyofanyika katika Mahakama kwa sasa pamoja na kutoa elimu hiyo kupitia mitandao inayoweza kuwafikia wananchi kwa urahisi.


"Silaha bora ya kupigania Haki ni kuelewa upatikanaji wa hiyo,  Haki unayopigania ipo chini ya Sheria, Kanuni au Taratibu ipi, hivyo kutokana na uelewa wa wananchi wengi, Taasisi hizo zinawajibu wa kuboresha mifumo ya kuwafikia wananchi, ili waweze kuwa na uelewa mpana zaidi namna bora ya kupata haki zao bila kuwa na migogoro" Amesema Mhe. Mongella.


Ameongeza kuwa, ikiwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mwendesha Mashtaka, Jeshi la  Magereza na Polisi pamoja na Taasisi zingine zinazojishughulisha na masuala ua kisheria zitaunganisha mifumo kupitia TEHAKA, licha ya kurahisisha upatikanaji wa haki, zaidi itaongeza uwezo wa wananchi kutambua namna bora na rahisi ya kupata haki zao.  


Aidha, ameipongeza Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, kwa huduma zilizotolewa kwa wananchi katika wiki ya Sheria, huduma ambazo ziliwanufaisha wananchi wengi wa mkoa huo, pamoja na kuwaunganisha na kuzifahamu Taasisi zinazojihusisha na Haki Jinai, jambo ambalo limeleta uhalisia wa dhima ya Siku ya Sheria nchini, inayomlenga mwananchi na wadau wa Sheria.


"Nikiri kuwa, licha ya wananchi zaidi ya laki moja kunufaika na elimu ya masuala ya kisheria na Haki Jinai, wananchi wananchi 516, waliopata msaada wa kisheria bure ni idadi kubwa ambayo, tunaamini wananchi hao wamepata amani ya mioyo na wanakwenda kuishi kwa amani na kujikita kwenye shughuli za uzalishaji mali, jambo ambalo linaimarisha amani na usalama wa mkoa wetu"Amethibitisha Mhe. Mongella.


Awali, Kilele cha Siku ya Sheria, kilitanguliwa na Maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini, yaliyofanyika kuanzia tarehe 24 - 30 Januari, 2024,  kwa kutoa Elimu kwa Umma na msaada wa Kisheria bure, kwenye viwanja TBA, eneo la Kaloleni, Jijini Arusha, yaliyobeba

Kauli Mbiu ya  "Umuhimu wa Dhana ya Haki kwa Ustawi wa Taifa; Nafasi ya Mahakama na Wadau katika Kuboresha Mfumo Jumuishi wa Haki Jinai"


#arushafursalukuki 




                        
                       
                        </div>
                        <!-- /.right-sidebar-content -->
                        <!--/END RIGHT SIDEBAR CONTENTE SECTION-->
                    </div>



<div class=

Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa