• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

SERIKALI YAANZA KUCHUKUA HATUA KUNUSURU UHARIBIFU WA DARAJA LA TENGANYETI LINALOUNGANISHA NCHI YA TANZANIA - KENYA..

Posted on: November 27th, 2023

Na Prisca Libaga - Arusha


Serikali imeanza kufanya matengenezo ya kwenye daraja kubwa la Tenganyeti na miundombinu ya kingo za barabara katika eneo la wilaya Longido, mkoa wa Arusha, daraja    linalounganisha nchi za Tanzania na Kenya, kufuatia uharibifu uliotokana na mvua zilizonyesha kwa zaidi ya saa saba, usiku wa kuamkia Novemba 25 huku  zikihatarisha kukata mawasiliano ya barabara kati nchi hizo, kupitia mpaka wa Namanga.


Serikali imeanza jitihada za kulinusuru daraja hilo,  lililopo kilometa chache kabla ya kuingia katika Kituo Jumuishi cha Forodha (OSBP- One Stop Border Post) cha Tanzania na Kenya cha Namanga, ambacho kimekuwa na shughuli nyingi za kuingiza na kutoa bidhaa kati ya nchi zote mbili.


Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania - TANROADS, Mhandisi, Mohammed Besta, amefika katika Daraja hilo na kutoa maelekezo kwa TANROADS Mkoa wa Arusha, kuendelea na jitihada za kulifanyia marekebisho daraja hilo, ili lisiendelee kuharibika zaidi.


Hata hivyo, Mhandisi Besta amewatoa hofu,  Watanzania, kuwa barabara zote nchini zipo salama na wamejipanga kukaniliana na uharibifu wowote utakaojitokeza kwa kipindi hiki cha Mvua.


"Kazi inayoendelea hapa, ni muendelezo wa kukabiliana na matukio ya   dharura kwa kipindi chote cha mvua, ni watake Mameneja wa mikoa yote kuwa tayari kukabiliana na uharibifu wa barabara utakaotokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini"Ameweka wazi Mhandisi Besta.


Kwa upande wake Meneja wa TANROADS, Mkoa wa Arusha, Mhandisi Reginald Massawe ametaja kuendelea na mikakati ya usanifu wa daraja hilo  pamoja na udhibiti wa mikondo ya maji, ili kunusuru daraja hilo kuendelea kuharibika.


Mkuu wa Wilaya ya Longido Marco Ng'umbi ameeleza kuwa, barabara hiyo ni umuhimu kwa wananchi na uchumi wa nchi zote mbili na Afrika Masharikia, hasa katika usafirishaji wa malighafi na bidhaa za kibiashara, ikiwemo mazao ya chakula.


"Sisi Mpaka wa Namanga ndio lango kuu la biashara, ikitokewa mawasiliano ya barabara yamekata, kutatokea athari kuwa, za kijamii na kiuchumi, kipekee tunaishukuru Serikali na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Kuijali Longido kwa kuboresha miundombinu ya barabara" Amesema Mhe. Ng'umbi

Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa