• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

SHULE YA MSINGI EMAIRETE YANUSURU WATOTO KUTEMBEA UMBALI MREFU.

Posted on: January 20th, 2024


Na Elinipa Lupembe

Shule mpya ya msingi Emairete kata ya Monduli Juu, ikiwa umbali wa Km 11 kutoka makao makuu ya wilaya hiyo, shule ambayo imeanza  Januari 08, 2024, ikiwa na wanafunzi 457 waliohamishiwa kutoka shule ya msingi Monduli Juu.

Mradi  huo, umetekelezwa kwa shilingi milioni 470, fedha kutoka Serikali Kuu kupitia Mradi wa Kuboresha Upatikanaji wa Fursa sawa katika Ujifunzaji Bora kwa Elimu ya Awali na Msingi Tanzania Bara (BOOST), umewaondolea mwendo wanafunzi wa kijiji cha Emairete, waliotembea umbali wa takribani Km 10 kwenda shuleni kila siku.

Wanafunzi hao, wameishukuru Serikali ya awamu ya sita, chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kujenga shule, ambayo wamekiri kuifurahia kutokana na ukweli kwamba, shule waliyosoma awali, ilikuwa mbali na kuwasababisha kutembea umbali mrefu huku  wengi wao walikosa masomo kutokana na makorongo kujaa maji, wakati wa msimu wa mvua.

Meleji Meshilo mwanafunzi wa darasa la 7, amekiri kufurahia kuhamishiwa shuleni  hapo, shule yenye majengo mazuri na ya kisasa, ikiwa karibu na nyumbani, jambo ambalo limewapunguzia mwendo, tofauti na awali walitembea umbali mrefu. 

"Wakati nasoma Monduli Juu,  nilikuwa mchelewaji, kila siku nilichelewa shule kutokana na umbali, nilianza kukata tamaa ya kusoma, kwa sasa nimeanza na ari mpya, nitasoma kwa bidii" Ameweka wazi Meleji

Naye Riziki Lesikar (7), amebainisha kuwa, mvua ikinyesha makorongo hujaa maji, na kuwalazimu kushindwa kwenda shule na kukosa vipindi vingi wakati wa msimu wote wa mvua.

"Tunamshukuru sana Rais wetu, Mama Samia, kwa kutujengea shule nzuri, madarasa ni mazuri, walimu wanatufundisha vizuri, mimi na wenzangu tunaahidi kusoma kwa bidii, natamani kufikia ndoto yangu ya kuwa daktari" Amesema Riziki

Hata hivyo, mwalimu Mkuu Msiadizi Mwl. Metui Saruni, ameweka wazi kuwa, shule ina jumla ya wanafunzi 457 darasa la awali mpaka la saba, ambao asilimia 90, wametokea shule ya msingi Monduli Juu.

Ameongeza kuwa licha ya kupunguza msongamano wa wanafunzi shule waliyotokea, pia wamepunguza kutembea umbali mrefu, shule mpya yenye miundombinu ya kisasa,  ina mazingira rafiki ya kufundishia na kujifunzia kwa walimu na wanafunzi.

Ikumbukwe kuwa, miradi hiyo ya ujenzi wa miundombinu shule za msingi ni utekelezaji wa Ilani ya CCM, Sura ya tatu Ibara ya 79 kifungu (q)Kukarabati miundombinu ya kufundishia na kujifunzia na kifungu (C) Kuboresha uratibu na usimamiaji wa stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu.







Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa