Baadhi ya wagonjwa waliojitokeza kupata huduma za afya kwenye Kambi ya Madaktari Bingwa na Wabobezi Mkoa wa Arusha, kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha mapema leo Juni 23, 2025
Ikiwa ni siku ya kwanza ya Kampeni ya siku saba iliyoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha chini ya Uongozi shupavu wa Mhe. Paul Christian Makonda kwa kushirikiana na wadau wengine wa sekta ya afya, wakazi wa mkoa huo na mikoa jirani wamejitokeza kupata huduma hizo za afya zinazotolewa bure.
Lengo la Kambi ya Matibabu haya ni kuwapa wananchi fursa ya kupata elimu ya afya, vipimo vya magonjwa mbalimbali na ushauri wa kitaalam ili kupata huduma stahiki za tiba na kinga ambapo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha inashirikiana na sekta binafsi, Hospitali na Taasisi mbalimbali za Matibabu.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa