Viongozi wa halmashauri wametakiwa kusimamia ujenzi wa vyumba vya madarasa ya sekondari hususani ya kidato cha kwanza kwenye maeneo yao haraka iwezekanavyo.
Maagizo hayo yametolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kwenye kikao cha ushauri cha Mkoa (RCC) kilichofanyika mapema wiki hii.
Amesema ni kweli Mkoa wa Arusha umeshika nafasi ya tatu (3) Kitaifa lakini bado kuna changamoto ya vyumba vya madarasa takribani 413 kwa Mkoa mzima wa Arusha.
Upungufu wa vyumbo hivyo vya madarasa ni 192 kwa Jiji la Arusha, 109 kwa Arusha DC, 37 kwa Meru, 32 kwa Monduli, Londigo 29 na Ngorongoro 33 ikiwa wilaya ya Karatu haina mapungufu hayo.
Hivyo kuwataka viongozi wa Wilaya, Halmashauri na wadau wa maeneo yao kushirikiana kwa karibu kuongeza vyumba hivyo kabla ya Januari ili watoto wote waliofaulu waweze kupata nafasi za masomo ya sekondari.
Akitoa taarifa ya elimu kwa Mkoa wa Arusha Katibu tawala upande wa Elimu bwana Gift Kyando, amesema Mkoa wa Arusha umefanya vizuri sana kwenye matokea ya darasa la saba kwa kushika nafasi ya 3 Kitaifa kati ya mikoa 26 na halmshauri ya jiji la Arusha imeshaka nafasi ya kwanza kati ya halmashauri 195.
Amesema mbali na ushindi huo bado mkoa unakabiliwa na changamoto ya mimba za mashuleni na upungufu wa matundu ya vyoo kwa baadhi ya shule za mkoani.
Hivyo juhudi kubwa bado inaitajika ili mkoa uweze kushika nafasi ya kwanza katika matokea yote ya mitihani.
Nae mbunge wa Ngorongoro mhe. Tate Wiliam Ole-Nasha ambae pia ni Naibu Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi, amesema ukiona mkoa unafanya vizuri kwenye mambo mbalimbali jua kuna viongozi wanaojituma na kuwajibika kwa ukaribu.
Kikao cha ushauri cha mkoa nicha kwanza kwa mwaka huu mpya 2018/2019 ambapo mambo mbalimbali yamejadiliwa kwa manufaa yakuongeza ufanisi katika shughuli za maendeleo ya mkoa.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa