• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

TANZANIA IMEENDELEA KUBAKI KWENYE HISTORIA YA KIDUNIA KWA KUWA NA UHUSIANO IMARA WA KIMATAIFA

Posted on: November 16th, 2023

Na Elinipa Lupembe.


Nchi ya Tanzania imeendelea kuweka historia ya kidunia kwa mahusiano mazuri ya Kimataifa na nchi nyingi duniani, mahusiano yanayozingatia maslahi ya kichumi, kijamii na mwendelezo wa Sera za ndani za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Hayo yamethibitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John V.K Mongella, wakati akifungua rasmi Kongamano la kukusanya Maoni ya wadau kuhusu marekebisho ya Sera ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001, kongamano lililofanyika kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC)  Jijini Arusha leo 13 Novemba, 2023.


Amesema kuwa, Sera ya Mambo ya Nje iliyopita ya mwaka 2001 imeleta mafanikio makubwa kwenye Nchi ya Tanznania, ikiwa ni pamoja na kudumisha mahusino mazuri na Nchi jirani, ukanda wa SADC na Kimataifa, kupitia misingi iliyowekwa na waasisi wa Taifa hilo,  hivyo ni vyema wadau hao kuichukulia kwa uzito unaostahil,i kwa msitakabali wa Nchi ya Tanzania kwa Miongo kadhaa mbele.


“Kutokana na unyeti wa Ajenda hii, washiriki wote kwa nafasi zenu mnalo jukumu la kuelewa mawasilisho yote hatua kwa hatua, ili kupata uwezo wa kuchangia kikamilifu mawazo, ambayo yatachakatwa mpaka ngazi ya Taifa, tumieni nafasi hii adhimu kwa manufaa ya Taifa letu”Ameweka wazi Mhe. Mongella


Hata hivyo, Mkurugenzi Msaidizi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Justine Kisoka, amesema kuwa, licha ya mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa Sera iliyopita, bado kunahitajika maboresho zaidi ili kukuza uhusino wa Kimataifa.


“Yapo mambo mapya ya kujumuishwa kwenye Sera hii, ili tuweze kunufaika zaidi kama Nchi, ikiwemo uchumi wa bluu ambao ni kipaumbele kwa nchi yetu ya Tanzania, pamoja na ushirikishwa wa watanzania waishio nje ya Nchi na raia wote wenye asili ya Tanzania waishio nchi nyingine ili waweze kujumuishwa katika kuchangia maendeleo ya Taifa lao”. Amesema Kisoka


Kwa upande wake Afisa wa Ofisi ya Rais Zanzibar, Salum Mohamed Ramia, amesema kuwa maoboresho ya Sera hiyo, ni kwa manufaa ya Watanzania wote, ikiwa imesheheni maeneo mengine mapya yenye kuleta tija huku Sera ya Uchumi wa bluu, ikiwa ni moja ya kipengele kitakachopewa kipaumbele.

Ikumbukwe kuwa, Sera hiyo ilitungwa mwaka 2001 na mchakato wake wa utekelezaji kuanza mwaka 2004 sasa inafanyiwa uboreshaji kwa kupokea maoni kutoka kwa wadau wa Sekta mbalimbali za binafsi na Umma.


#mahusianoyakimataifa

#uchumiwabluu

#arushafursalukuki

Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa