• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

TANZANIA INATEKELEZA TAMKO LA AMANI KATIKA NCHI ZA UKANDA WA MAZIWA MAKUU; TAMKO LA DAR ES SALAAM

Posted on: October 27th, 2023


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imeendelea kuchukua hatua katika kutatua migogoro mbalimbali na kutekeleza kwa vitendo Tamko la Dar es Salaam kuhusu Amani, Usalama, Demokrasia na Maendeleo katika Ukanda wa Maziwa Makuu.

Hayo yamebainishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Kawaida cha 77 cha Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, leo Oktoba 20,2023 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) jijini Arusha.

“Kwa mfano, hivi sasa Tanzania inashiriki katika Jeshi la Umoja wa Mataifa, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (Stabilization Mission) na Jeshi la Kulinda Amani (MONUSCO)” ameomgeza Dkt. Mwinyi.

Aidha, Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa, katika kuepusha uvunjifu wa haki za binadamu unaotokana na vita, kupitia Jumuiya ya Afrika Mashariki, Tanzania inashiriki katika Jeshi la pamoja la kulinda amani madhariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na pia imeshiriki katika ulinzi wa amani katika nchi mbali mbali ikiwemo huko Darfur Sudan na Visiwa vya Comoro.

“Naona fahari kwa Majeshi yetu kwa kazi yao nzuri wanayoifanya; nitoe wito kwa nchi zetu za Afrika kuendelea kushirikiana katika kuyakabili matukio mbalimbali yanayohitaji msaada wa kibinadamu katika Bara letu” ameongeza Dkt. Mwinyi.

Kwa upande wake, Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Pindi Chana, amebainisha kuwa, Kikao hicho cha 77 cha Kamisheni za Haki za Binadamu na Watu kimelenga kujadili na kubadilishana uzoefu katika kusimamia masuala ya haki za binadamu na watu.

Aidha, ameongeza kuwa Tanzania ipo tayari kushirikiana na Afrika nzima kama jinsi ambavyo imekuwa ikishirikiana nao tangu enzi za uongozi wa Awamu ya Kwanza chini ya Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

“Utaratibu wa kutambua haki za binadamu nchini Tanzania umekuwa ni utamaduni tangu enzi za Mwalimu Julius Nyerere wakati nchi inapata uhuru. Tutakuwa na wajibu wa kuhakikisha ndugu na majirani zetu ndani ya Afrika wanapata uhuru” amebainisha Balozi Dkt. Chana.

Nae Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar, Mhe. Haroun Ali Suleiman ameeleza kuwa Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi, anatekeleza kwa vitendo masuala ya Sheria, Utawala Bora na Haki za Binadamu na pia ameendeleza huduma mbalimbali za elimu, afya, maji na miundombinu kwa ajili ya wananchi.

Takribani wadau 1000 wa masuala ya haki za binadamu wanashiriki Kikao cha Kawaida cha 77 cha Kamisheni ya Haki za Binadamu na Watu kutoka Serikali za Afrika, Wawakilishi kutoka Umoja wa Mataifa, Wawakilishi kutoka Umoja wa Afrika, Taasisi za Kitaifa za Haki za Binadamu, Mabalozi kutoka nchi mbalimbali, Asasi za Kiraia, Viongozi wa Kidini na kimila na watu wengine.

Mwisho.




Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa