• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

TARURA IMEJIPANGA KUBORESHA MTANDAO WA BARABARA

Posted on: September 4th, 2024


Arusha



Wakala ya Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA) imejipanga kuboresha mtandao wake wa barabara kwa kuziwekea lami na nyingine changarawe kwa viwango ambavyo zitadumu kwa muda mrefu kutokana na bajeti ya wakala huo kuongezeka zaidi ya mara tatu.



Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Wakala huo Mhandisi Florian Kabaka wakati akiongea na waandishi wa habari katika maonesho yanayoendelea viwanja vya AICC jijini Arusha  kwenye kikao kazi cha Wenyeviti na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma ulioandaliwa na Ofisi ya Msajili wa hazina.



“TARURA tutaendelea kujenga barabara kwa nguvu zaidi kwani  katika miaka mitatu hii kiwango cha bajeti kimepanda zaidi ya mara tatu na hii inatuwezesha kuwa na uwezo wa kuhudumia barabara zetu kwa ubora.Tunamshukuru sana Mhe. Dkt. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutuongezea bajeti kila mwaka. 



Amesema kutokana na ongezeko la bajeti hiyo wameweka mipango ya kuboresha mtandao wa barabara kila mwaka kwa kuingiza barabara za changarawe kuwa katika kiwango cha lami pia barabara za udongo kuwa kiwango cha changarawe zenye ubora.



Kwa upande wa maabara ya TARURA, Mhandisi Kabaka ameongeza kusema kwamba  itaendelea kuhakikisha miradi inayotekelezwa  inakuwa yenye viwango  na ubora kwa kupima malighafi zote zinazohusika katika ujenzi wa miundombinu kabla ya kuanza ujenzi na matengenezo ili kuepuka ujenzi wa viwango vya chini.



Naye, Mhandisi Mshauri Pharles Ngeleja kutoka TARURA Makao Makuu  amesema  mtandao wa barabara wa Wakala huo ni mkubwa sana hivyo wameamua kutumia teknolojia mbadala ili kuweza kufungua barabara nchi nzima ndani ya kipindi kifupi.



Amesema hadi sasa wameweza kujenga barabara za teknolojia mbadala Km. 28 ambazo zimejengwa katika mikoa ya Mwanza, Kigoma, Rukwa pamoja na Morogoro na bado wanaendelea kujenga maeneo yote ambayo rasilimali inapatikana eneo husika.



Kwa upande wa madaraja amesema tayari wanajenga madaraja kwa kutumia mawe na madaraja hayo ni imara na hivyo kuwafungulia wananchi  kuweza kutumia na kuwarahisishia kupata huduma  mbalimbali muhimu kwenye maeneo yao pamoja na kuwafungulia uchumi kwa kufika kiurahisi kwenye masoko.


Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa