• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

TAWTO WAKARABATI JENGO LA OFISI YA POLISI DAWATI LA JINSIA ARUSHA.

Posted on: February 13th, 2024


Chama cha wanawake Mawakala wa Utalii Tanzania (TAWTO) wamekarabati Jengo la Ofisi ya Polisi Masuala ya Jinsia na watoto, Wilaya ya Arusha na Kumkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John V.K Mongella.


Jengo hilo, lililokuwa uchakavu kutokana na kujengwa kwa muda mrefu, lilepambwa kwa michoro inayovutia ya wahanga wanaofanyiwa ukatili kueleza zaidi changamoto wanazokumbana nazo kwenye jamii pamoja na kuwekwa samani za ofisi.


Akikabidhi jengo hilo Jijini Arusha, Mwenyekiti wa TAWTO, Elizabeth Ayo amesema chama hicho kimeona umuhimu wa kukarabati jengo la Dawati hilo, litakalosaidia katika kusimamia na kulinda haki za wanawake na watoto pamoja na watoa huduma ambao ni Jeshi la Polisi.


"Tumeamua kuunga mkono juhudi za Serikali kwa fedha kidogo tuliyojaliwa kama chama ili jamii hususani wanawake na watoto waweze kupata haki kwenye mazingira rafiki kwa wahusika". Amesema.


Akizungumza wakati akikabidhiwa jingo hilo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. JOHN V.K Mongella, amewashukuru wadau hao kwa kujitolea kusadia kuboresha mazingira ya utoaji huduma kwa jamii kupitia Dawati hilo la Jinsia kwani wanafanya mambo makubwa katika kuhakikisha uchumi wa nchi unakua kupitia sekta ya utalii.


"Hiki mlichofanya Mungu atawalipa sababu kuna watu wanataabika na unyanyasaji ikiwemo ukatili kwa watoto, wanawake na wanaume ambapo sasa ukarabati huu utatoa ari zaidi katika kutafuta suluhu ya changamoto za ukatili ikiwemo kulinda haki za watoto na kinamama".


Hata hivyo Mhe. Mongella ametoa rai kwa wananchi wote kutojihusisha na vitendo vya kikatili kwa makundi yote na kusababisha madhara ya kisaikolojia kwani hatua za kisheria zitaendelea kufuata mkondo wake ili kudhibiti matukio hayo huku akitoa wito kwa wadau wa maendeleo kuiga mfano wa Taasisi hiyo kwa kujitokeza na kutoa michango yao kusaidia jamii.


Akisoma taarifa fupi, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi ambaye ni Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Wilaya ya Arusha, Ursula Mosha amesema dawati  la Jinsia na watoto ni dawati lenye kusaidia jamii kuhusu kupinga unyanyasaji wa kijinsia wanaofanyiwa wanawake, watoto na wanaume ambapo Awali dawati hilo lilianzishwa mwaka 2010 kwa kuhudumia jamii na kushauri dhidi ya ukatili.


Amesema kuwa dawati hilo linatoa  huduma ya ushauri kwa wanandoa ikiwemo elimu na makuzi, kuunganisha familia zilizotengana pamoja, ushauri wa usiri kwa wahanga wa ukatili katika Dawati la Jinsia la Huduma kwa Pamoja lililopo Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru ikiwemo utoaji wa elimu kwa jamii.


Pia Alishukuru TAWTO kwa kusaidia ukarabati wa jengo hilo lililokuwa chakavu kwa kupewa meza tano za kisasa,viti kumi na mabenchi matatu ikiwemo marekebisho ya upakaji rangi,paa sakafu ikiwemo michoro ya kuhamasisha watoto wanapofika dawati kutoa changamoto zao za ukatili.


"Tunalengo la kuwa na jengo huru ili kutoa uhuru kwa wahanga wanaofanyiwa ukatili na pia michoro itakapokamilika tunawaomba wadau wajitokeze zaidi kuchangia dawati hilo tunawashukuru sana TAWTO kwaukarabati huu"


Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA AFUNGUA MKUTANO WA 33 WA WAKUU WA MAJESHI YA ULINZI (SADC).

    May 30, 2025
  • SAMIA MOTOCROSS CHAMPIONSHIP KUREJEA MSIMU WA PILI JULAI 12, 2025

    May 27, 2025
  • MKOA WA ARUSHA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO MKUBWA WA WAKUU WA MAJESHI WA SADC

    May 25, 2025
  • UJENZI WA UWANJA WA AFCON ARUSHA SIO MICHEZO TU, NI FURSA YA KIUCHUMI

    May 24, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa