Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) imeanza kutumia mitambo na vifaa vya kisasa vya kielektroniki, kukagua na kutambua changamoto za magari jambo ambalo licha ya kuokoa mugpda na gharama limeongeza ufanisi katika utendaji wa kazi na utoaji huduma.
Akitoa maelezo mbele ya Waziri Mkuu Jamhuri ya Muungano Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Mhandisi wa Mitambo Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mustafa Abdul amemuelezea kuwa, TEMESA imeanza kutumia vifaa vya kisasa vya kielekroniki katika ukaguzi wa mfumo wa umeme na injini za magari.
Amebaibisha kuwa, kwa sasa TEMESA inavyo vifaa vya kielekroniki vyenye uwezo wa kukagua mifumo ya umeme na injini kwenye gari, mitambo ambayo inauwezo wa kutambua tatizo lilipo bila kulifungua pamoja na kuonyesha matengenezo yanayohitajika.
"TEMESA kwa sasa inatumia vifaa mbavyo vinakagua gari bila kulifungua na kutambua changamoto zinazoikabilia gari na matengenezo yanayohitajika jambo ambalo linarahisisha kazi kwa kuokoa muda na gharama, ukaguzi wake ni wa uhakika na unakupeleka moja kwa moja kwenye tatizo tofauti na zamani mafundi walikuwa wanakisia kama wapiga ramli" Amesema Mhandisi Mustafa
Aidha amefafanua kuwa, vifaa hivyo vya kisasa kwa sasa vipo kwenye ofisi za TEMESA kwenye mikoa yote Tanzania nzima jambo ambalo limeboresha kwa kiasi kikubwa utendaji wa kazi katika kutoa huduma kwenye Taasisi za Umma na Serikali.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa