• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

TIMU YA SAMIA LEGAL AID YATIA KAMBI ARUSHA: MAOFISA WA SERIKALI WANAOPINDISHA HAKI KUSHUGHULIKIWA

Posted on: March 27th, 2025

Timu ya watoa huduma wa msaada wa Kisheria kupitia kampeni ya "Samia Legal Aid Campaign " imeagizwa kuorodhesha majina ya watumishi wa serikali katika sekta mbalimbali watakaobainika kutajwa na wananchi kuwa wanachochea migogoro inayopelekea wananchi kuichukia Serikali. 



Maagizo hayo yametolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.  Paul Christian Makonda wakati akiongea na wataalam wa sheria wakiwemo mawakili, maofisa maendeleo ya jamii pamoja na wakuu wa idara na vitengo mbalimbali waliokutana kwaaajili ya kupanga mikakati ya utatuzi wa changamoto za wananchi katika halmashauri saba za Mkoa wa Arusha pamoja na kuainisha changamoto zinazopaswa kufanyiwa kazi katika kila idara husika. 



Amesema kunabaadhi ya maofisa maendeleo ya jamii wanalalamikiwa kwa kupindisha sheria ikiwemo watumishi wengine hivyo katika kampeni hiyo endapo kuna watumishi wanalalamikiwa kukwamisha utatuzi wa migogoro kwa wananchi  wakuu wa timu husika kutoka Wizara ya Katiba na Sheria waandike majina yao kisha mwisho wa kampeni hiyo watoe taarifa kwake ili hatua stahiki zichukuliwe. 



"Kuna baadhi ya watumishi wanatajwa na wananchi kutokana na tabia ya kukwamisha mambo tunaomba majina yao, lakini pia naomba timu hizi zianishe changamoto zote zilizoibuka ili kupelekwa mahali husika kama polisi, uhamiaji, idara ya kazi na kwingineko ili hatua stahiki zichukuliwe "



Hata hivyo, amewasihi watoa huduma hiyo kuhakikisha wanawasilikiliza wananchi wanaofika kupata msaada huo  ikiwemo watoa huduma hao kujiuliza nafsini kwao je maamuzi watakayotoa ni sahihi na hakuna upendeleo ili wahusika wapate haki yao kwamujibu wa changamoto zao. 



Kwa upande wake Ester Msambazi ambaye ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Msaada wa Kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, amesema kampeni hiyo ilianza kutekelezwa mwaka 2023 huku Mkoa wa Arusha ukiwa ni wa 23 tangu kampeni hiyo kuanza na wamejipanga vema kuanza kutoa msaada huo.



Uzinduzi wa kampeni hiyo utafanyika Machi 28, 2025 kwenye viwanja vya Ngarenaro ambapo Waziri wa Katiba na Sheria, Dk, Damas Ndumbaro na Mhe. Makonda watahudhuria huku huduma na elimu za kisheria zikitolewa, utoaji wa huduma za Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Polisi pamoja na idara na ofisi mbalimbali za serikali ambazo zitatoa huduma za bure kwa wananchi na baada ya hapo timu husika zinaenda uwandani kuanza kazi rasmi Machi 29,mwaka huu.


Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa