Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Dkt. Athumani Kihamia amezitaka Halmashauri zote za Mkoa wa Arusha kuhakikisha zinafuta haraka madeni yote madogo madogo.
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza kwenye kikao cha kujadili hoja za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.John Mongella.
"Hakuna haja ya kulimbikiza madeni haya madogo madogo yanaongeza hoja zisizo na ulazima".
Aidha, imeipongeza halmashauri hiyo kwa kufanya vizuri katika matumizi ya fedha kwa mwaka 2019/2020.
Amewataka waendelee kusimamia vyanzo vyao vya mapato vilivyopo kwa sasa na kuongeza vingine vipya ili kuongeza wigo wa mapato ya ndani.
Aidha,Mwenyekiti wa halmshauri ya Meru Mhe. Jeremiah Koshili amewashauri pia madiwani kufanya semina elekezi kwa vikundi vya mikopo vya akinamama katika kata zao kabla hawajapatiwa mikopo.
Dkt.Kihamia ameendelea na vikao vya kujadili hoja za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali katika halmashauri za Mkoa wa Arusha huku akiambana na baadhi ya Maafisa kutoka katika ofisi yake.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa