"Tumieni michezo kudumisha umoja wetu ili uwe imara zaidi na kuleta mshikamano".
Kauli hiyo imesemwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa, alipokuwa akifungua michezo ya mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Jijini Arusha.
Lengo la michezo hiyo ni kudumisha umoja, uhusiano wa nchi za Jumuiya hiyo.
Vile vile michezo hiyo inasaidia kujenga Afya na nichanzo cha ajira kwa vijana wengi, hivyo amewataka wabunge hao kwenda kuhamasisha michezo katika nchi zao.
Aidha, amewashauri wabunge hao kutumia fursa hiyo ya kukutana pamoja na kubadilishana mawazo ya namna ya kuimarisha umoja huo.
Spika wa bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhe. Mathias Ngoga amesema michezo hiyo inaleta mshikamano baina ya wabunge huo na hata nchi zao.
Amewataka wabunge hao kupitia michezo hiyo waendeleze malengo yaliyowekwa na Jumuiya hiyo.
Akizungumza pia, Naibu spika wa bunge la Jumhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson, amesema kukutana kwa wabunge hao kuwe njia moja wapo ya kuweza kujadili changamoto za wananchi wao na namna ya kuzitatua.
Mhe. Sarah Opendi mbunge kutoka bunge la Uganda akimwakilisha Naibu spika wa bunge hilo amesisitiza kupitia michezo hiyo wabunge wote wapaze sauti zao kupiga vita ukatili wa wanawake na watoto katika nchi zao.
Michezo hiyo ya mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yamejumuisha watu zaidi ya 1500 kutoka katika nchi ya Tanzania bara na visiwani, Kenya, Uganda na Burundi na mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika Jijini Arusha kwa wiki 2.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa