Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Dkt. Athumani Kihamia amezitaka taasisi za Serikali Mkoani Arusha kufanya kazi kwa umoja na mshikamano ili Arusha iweze kusonga mbele.
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Viongozi wa taasisi mbalimbali za Serikali za Mkoa wa Arusha.
Aidha, amezitaka taasisi hizo kuwa zinatoa taarifa zake za kiutendaji na kuziwasilisha katika ofisi yake.
Amesema ushirikiano ukiwepo hata migongano ya hapa na pale haitakuwepo kwani kila mmoja atajua majukumu ya mwenzake na kuyaheshimu.
Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na usimamizi wa mazingira (NEMC) Mkoa wa Arusha bwana Laurance Nzari, amesema kikao hicho kimekuwa chachu yakuleta umoja na ushirikiano baina ya Ofisi ya Mkoa na taasisi hizo.
Bwana Nzari amesisitiza kuwa uhusiano mzuri utasaidia kupunguza gharama za uwendeshaji baina ya taasisi hizo.
Nae, Kaimu Mkurugenzi kutoka taasisi ya utafiti wa Kilimo Tanzania(TPRI) Dkt. Efrem Njau amesema kikao hicho kimetoa mwelekeo wa namna wanatakiwa kufanya kazi kwa pamoja.
Kikao hicho kimefanyika kwa mala ya kwanza katika Mkoa wa Arusha kwa lengo la kuhakikisha ofisi ya Mkoa na taasisi hizo zinafanya kazi kwa pamoja.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa