. Aipongeza CRDB kwa kufikisha Miaka 30 ya kuwahudumia Watanzania katika maeneo mengi ikiwemo Namanga
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla leo Ijumaa Septemba 26, 2025 amezindua Tawi la Benki ya CRDB, Namanga Wilayani Longido, akisema tawi hilo litakuwa kiunganishi muhimu cha biashara za mpakani, kukuza biashara pamoja na kuimarisha uchumi wa Kikanda suala ambalo litaifanya Namanga kuendelea kuwa kitovu cha biashara, Kilimo na uwekezaji.
"Serikali pia imeendelea kuwekeza katika miundombinu ya TEHAMA ikiwemo kuimarisha Mkongo wa Taifa wa mawasiliano na kuweka mazingira rafiki ya ubunifu kama vile huduma za kibenki za kidijitali, huduma za fedha kupitia simu, huduma za kibenki mtandaoni na pia huduma za uwekezaji kama kijani bond, Samia infrastructure bond na SUKUK ambazo benki ya CRDB imeongoza katika kuanzishwa kwake." Amekaririwa akisema CPA Makalla.
Amesema huduma hizo za kifedha ni kichocheo muhimu cha ustawi wa wananchi na maendeleo ya Taifa, ikisaidia kuwezesha wananchi kuweka akiba kwa njia salama, kupata mikopo ya kuendeleza biashara na shughuli zao nyingine za kiuchumi na kushiriki kujenga uchumi na kupunguza umaskini, akiwataka kuunganisha huduma zao na sekta ya utalii kwa kupeleka huduma kwenye maeneo yenye kutembelewa zaidi na watalii na wageni wanaofika Mkoani Arusha.
Akitoa maelezo ya Benki hiyo kwa Mkuu wa Mkoa, Mkurugenzi wa Wateja wadogo na wa Kati Bw. Bonaventura Paul amesema Benki hiyo itaendelea kuwa Mshirika wa Kimkakati wa maendeleo ya Mkoa wa Arusha ambapo kufunguliwa kwa tawi la Namanga kunaifanya benki hiyo kuwa na Jumla ya matawi 14 miongoni mwa matawi 268 nchi nzima, wakiwa na mawakala 1801 kwenye Mkoa wa Arusha, 120 kati yake wakiwa Wilaya ya Longido.
Kwa upande wake Meneja wa Benki hiyo Kanda ya Kaskazini Bw. Cosmas Saddat amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuweka mazingira bora ya ufanyaji wa biashara kwa Taasisi za kifedha nchini pamoja na ushirikiano mkubwa wanaoupata serikalini, akiwahakikishia wananchi wa Namanga na Wilaya ya Longido kuwa kwasasa huduma za Benki hiyo zinapatikana kwa asilimia
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa