Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda ametembelea na kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa uwanja wa AFCON unaoendelea kwenye Kata ya Olmot, Halmashauri ya Jiji la Arusha.
Katika ziara hiyo iliyofanyika leo 24 Mei, 2025, Mhe. Makonda amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuona Mkoa wa Arusha unafaa kuwa sehemu ya michezo ambayo ni sehemu ya kukuza uchumi kwa wakazi wa Mkoa huo pamoja na Taifa kwa ujumla.
Mkoa wa Arusha unatarajiwa kuwa miongoni mwa wenyeji wa mashindano ya kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2027
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa