"Takwimu za mwaka 2016 zinaonesha magonjwa yasiyoambukiza yanachangia vifo vya watu zaidi ya Milioni 41 sawa na 71% ya vifo vyote, nchini".
Kauli hiyo imesemwa na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul alipokuwa akifungua maadhimisho ya wiki ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza kitaifa yanayofanyika Mkoani Arusha.
Amesema magonjwa haya yanaanza katika umri mdogo sana na hivyo kudhorotesha nguvu kazi katika Jamii.
Hivyo ameitaka Jamii yote kuzingatia ufanyaji wa mazoezi ya mwili kila mara ili kuweka mazingira rafiki ya afya zetu ikiwemo kuzuia magonjwa kama ya Kisukari, shinikizo la juu la Damu, msongo wa mawazo, pumu, sikoseli, kinywa, Koo na mengine mengi.
Mhe.Gekul amesema Serikali imetenga siku ya Jumamosi ya wiki ya pili ya kila mwezi iwe siku maalamu yakufanya mazoezi ya mwili,hivyo amesisitiza watu wote hasa wenye majukumu ya kukaa chini muda mrefu kufanya mazoezi mara kwa mara hasa watumishi wa Serikali, sekta binafsi na wanafunzi ili kujikinga na magonjwa hayo.
Mkurugenzi wa idara tiba kutoka Wizara ya Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Vivian Wonanji amesema Wizara hiyo imeandaa muongozo unaonesha namna yakulinda afya za watu katika makundi mbalimbali.
Amesema lengo la muongozo huo nikuwahamasisha watu katika sekta mbalimbali kuacha tabia bwete( kutofanya mazoezi) na muongozo huo umelenga kuanzia umri wa miaka 5 hadi 64.
Nae, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.John Mongella amesema wiki hii ya maadhimisho itafana sana kwani Mkoa wa Arusha umepewa jukumu la heshima.
Maadhimisho hayo yamefinguliwa rasmi Novemba 6 na yanatarajiwa kufungwa Novemba 13 na Mhe. Dorothy Gwajima na Novemba 10 utafanyika uzinduzi wa maonesho mbalimbali na Novemba 11 na 12 kutakuwa na Kongamano la Kisayansi.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa