• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

VIJANA KARATU WAISHUKURU SERIKALI YA MAMA SAMIA KWA MIKOPO ISIYO NA RIBA; YAWAWEZESHA KUANZISHA KIWANDA CHA KUOKA VITAFUNWA....

Posted on: October 18th, 2023

VIJANA KARATU WAISHUKURU SERIKALI YA MAMA SAMIA KWA MIKOPO ISIYO NA RIBA; YAWAWEZESHA KUANZISHA KIWANDA CHA KUOKA VITAFUNWA.


Na Elinipa Lupembe


Vijana wa Kikundi cha Amani Barazani Youth Group cha wilaya ya Karatu, wameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwathamini vijana wakitanzani na kuwatengenezea fursa za kujiinua Kiuchumi zinazowaweesha kujiajiri na kuajiri vijana wengine.


Mwenyekiti wa kikundi hicho, James Emmanuel amesema kuwa kukundi kina wanachama 10 na kilianza mradi wa kupika maandazi kwa mtaji kwa kuchangishana fedha kupitia kikundi chao cha kuweka na kukopa na baadaye kuwezeshwa na ofisi ya mkurugenzi halmashauri ya Karatu kwa kupata mkopo usiokuwa na riba wa shilingi milioni 8 kwa awamu mbili.


Fedha hizo ziliwawezesha kukuza mtani na kununua jiko kubwa la kuokea vitafunwa na kuanza kuoka mikate na keki, biashara ambayo inaendelea kukua na kushamiri wakiwa wameliteka soko la vitafunwa wilaya ya Karatu na vitongoji vyake.


Mwenyekiti huyo ameweka wazi kuwa awali waliposikia habari za mikopo hawakuamini, wakidhani ni mambo ya siasa, lakini baada ya kukutana na watalamu na kuwapa elimu ya mikopo na ujasiriamali, taratibu zote na hatimaye  kupata mkopo, ndipo walipoamini Serikali ya mama Samia iko makini na ina mikakati imara kuhusu vijana.


"Kupitia biashara hii, licha ya kutuinua kiuchumi imetuwezesha kujiari na kuajiri vijana wengine 13, vijana 6 wakiwa na ajira rasmi na vijana 7 vibarua kazi za muda, zaidi imetuwezesha kukutana na wadau wengi wanaondelea kutupa uzoefu wa kukua katika masoko na kukuza biashara yetu"Amesema Emmanuel.


Aidha amewasihi vijana wengie kutumia fusra hiyo adhimu kwa kuwa kunao utofauti mkubwa kati ya mikopo inayotolewa na serikali na ile ya benki yenye riba kubwa hasa ukizingatia vijana wengi hawana vigezo vya kuweza kukopeshwa na benki, sheria zao zinamuhitaji mkopaji kumiliki mali zisizohamishika ambazo kimsingi vijana hawana.


Ameongeza kuwa licha ya kuwa soko la vitafunwa linaushindani mkunwa lakini kutokana na ubora wa bidhaa zao zimeweza kupenya  sokoni na kupokelewa kwa mwitikio mkubwa unaowafanya kutamani kumiliki kiwanda kikubwa kitakachozalisha bidhaa nyingi zitakazopatikana Karatu na vitongoji vyake  na hatimaye maneneo mengine nje ya Karatu na ikiwezekana mkoa wa Arusha na Tanzania nzima.


Hata hivyo wameishukuru Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha, kwa uongozi wa Mhe. John V.K. Mongella kwa fursa nyingi anazozitoa kwa vijana kwa kuwakutanisha na watalamu, wadau na wateja pinda yanapotokea maonesho makubwa yanayohusu vijana na biashara, fursa ambazo zinawawezesha kubadilishana uzoefu, kutambua fursa zaidi pamoja  na kukua kibiashara.


#ArushaFursaLukuki

#KaziInaendelea









Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa