• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

VIKUNDI VYA VIJANA WAJASIRIAMALI ARUSHA WAISHUKURU SERIKALI KWA KUWEKA MAZINGIRA RAFIKI YA VIJANA  KUJIAJIRI....

Posted on: October 14th, 2023

Na Elinipa Lupembe


Vikundi vya vijana wajasiriamali mkoani Arusha wameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuweka mazingira rafiki yanayowapa fursa vijana kuwa wabunifu kupitia rasilimali rahisi zinazopatikana kwenye mazingira yao na kujiari pamoja na kuajiri vijana wenzao.


Vijana wayasema haya wakati wa maonesho ya  Wiki ya vijana kitaifa, yaliyofanyika kwenye viwanja vya Stendi ya Zamani Babati mkoani Manyara yaliyohusisha ubunifu, utangazaji na uuzaji wa bidhaa zao.


Mwenyekiti wa kikundi cha  

Grin Makers Solution Tz, kinachofanya shughuli zake, halmashauri ya Arusha wailaya ya Arumeru, Bartazari Ansen Twati amethibitisha kuwa baada ya kikundi hicho kuwa na wazo la kutengeza mashine za kufyatulia matofali watalamu wa serikali walipokea wazo hilo na kuwaunganisha na wadau wa sekta nyingine jambo ambalo limewawezesha kuwa na kiwanda kidogo cha kutengeneza 'paving blocks' za plastiki kwa kutumia taka za plastiki.


"Tulipoanzisha wazo letu, tulikuwa na hofu lakini serikali imetushika mkono kwa kuanza biashara na kufanya mchakato wa kusajili kiwanda chetu, kupata vibali vyote vya uzalishaji pamoja na kutuweka kwenye mchakato wa kupata mkopo kupitia Mfuko wa Vijana Ofisi wa Waziri Mkuu, tunategemea kupata mkopo mkubwa wa kuendesha na kuongeza uzalishaji katika kiwanda chetu" Amesema Twati.


"Tunamshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa fursa za sekta mbalimbali zilizofunguliwa kwa vijana wa kitanzania, ambazi zimewapa ujasiri  vijana wengi kuthubu kujiajiri huku wengi wakipata mafanikio makubwa ya kichumi na kijamii"


Naye James Emmanuel Mwenyekiti wa kikundi cha Amani Barazani kinachojishughulisha na ukoji wa vitafunio wilayani Karatu, amesema kuwa kupitia mikopo isiyokuwa na riba inayotolea na halmashauri, wameweza kubadilisha biashara yao kutoka kupika maandazi na kununua mashine ya kuokea vitafunioa vya aina zote.


"Mwanzo hatukuamini kuhusu mikopo isiyokuwa na riba, tulidhani ni ubabaishaji tuu, lakini tulipewa elimu ya mikopo hiyo na hatimaye kukopeshwa shilingi milioni 8 fedha ambazo zimetuwezesha kununua 'oven' na mashine nyingine za kukandia unga" Ameweka wazi James


Sara Lazaro Mwenyekiti wa kikundi cha Emanyata Youth Group cha wilayani Longido wanaojihusisha na utengenzaji wa urembo kwa kutumia shanga, amesema kuwa  zamani ilikiwa sio rahisi kuwa kabila la Kimaasai kuwakutanisha vijana wa kike na kiume kufanya kazi pamoja, serikali imefanya kazi kubwa sana ya kutoa elimu na kuwaunganisha vijana wa jinsi moja na sasa wanafanya kazi pamoja kama timu.


"Kila mtu alikuwa tunatengeza bidhaa zake mwenyewe kupitia serikali tumeweza kuungana na kupewa mkopo wa milioni 8, fedha ambazo licha ya kuonheza mitaji kwenye biasha zetu, umetuwezesha kununua mashine ya kusaga na kukoboa nafaka, kazi ambazo zimeweza kutuongezea vipato na kukuza uchumi wa familia kwa maendeleo ya Taifa letu" Amesema Sara


Hata hivyo Kaimu Afisa Vijana mkoa wa Arusha , Hanifa Ramadhani amesema kuwa serikali ya awamu ya sita inayo mikakati mingi kisekta ya kuwajengea uwezo vijana wa kujiajiri licha ya kuwa na programu tofauti za kuwapa mikopo ya kukuza mitaji zipo programu nyingine za kuwapa elimu ya kujiajiri, kufanya biashara, kuweka na kukopa, kukuza mitaji,  kupata vibali vya biashara zao ikiwa ni pamoja na kusajili vikundi, kusajili biashara, kulipa ushuru, kodi na tozo za serikali kwa kuwaunganisha kwenye Mamlaka husika.


"Serikali inawasimamia vijana kuweza kujiajiri kwa kiwapa mikopo siyokuwa na riba inayotolewa na halmashauri, upo Mfuko wa Ofisi ya Waziri Mkuu, programnya Kilimo BBT, imasimamiwa na wizara ya Kilimo,program za Jeshi la Kujenga Taifa zote zina lengo la iwajengea uwezo wa kujitegemea katika kulitumikia Taifa la Tanzania" Amefafanua Afisa Vijana huyo


Maonesho ya wiki ya Vijana Kitaifa yamehitimishwa leo ikiwa ni kumbukizi ya Kifo cha Hayati Baba wa Taifa Mw. Julius Kambarage Nyerere na Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 yenye Kauli mbiu ya Vijana na Ujuzi Rafiki wa Mazingira kwa Maendeleo Endelevu.


#Arushafursalukuki

#kaziinaendelea










Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa