• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

VIONGOZI WA CHAMA NA SERIKALI; WAZUNGUMZIA UADILIFU NA UTIIFU WA ZELOTHE...

Posted on: October 30th, 2023

Na Elinipa Lupembe


Viongozi wa Chama na Serikali waliopata fursa ya kuzungumza wakati wa ibada ya mazishi ya aliyekuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi (mstaafu) wa Jeshi la polisi nchini na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha, Marehemu Zelothe Stephene Zelothe kuwa alikuwa ni kiongozi mwadilifu na mwenye nidhamu, aliyewapenda anaowaongoza na asiyependa makuu.


Viongozi hao licha ya kuhuzunishwa na kifo cha Zelothe lakini wamekiri kuendelea kuyaishi maisha ya yake, maisha ambayo wengi wametoa shuhuda za kuwa alikuwa mwenye nidhamu, muadilifu na mtiifu kwa watu wa kila rika.


Makamu Mwenyekitia wa CCM Taifa Tanzania Bara Abdulrahman Kinana, amesema kuwa, Zelothe alikuwa kiongozi mwenye uwezo wa kuongoza bila kujali mamlaka na vyeo alivyokuwa navyo kwa kuwa alikuwa mnyenyekevu na mtiifu kwa wengine.


Ametoa mfano alioutoa  Hayati baba wa Taifa Mwl.JK Nyeree, kuwa uongozi ni tabia sio usomi wala elimu, kinachomtofautisha kiongozi na watu wengine ni tabia na sio wadhifa alionao, tabia ambazo amekiri alikuwa nazo Zelothe licha ya kuwa na nyadhifa kubwa serikalini na kwenye Chama alikuwa ni mnyenyekevu na mwadilifu mwenye kufanyakazi kwa kuweka mbele uzalendo.


"Wapo wasomi wameshindwa kuwa viongozi wazuri na wapo wasiosoma wamekuwa viongozi wazuri, Zelothe alishika uongozi kwa nyadhifa nyingi na za juu serikalini lakini hukuwahi kuwa na majivuno, aliendelea kuwa mnyenyekevu kwa watu anaowaongoza na watu wa kawaida, hii ni tabia ya kuigwa na viongozi wengine tuliobaki" Amebainisha Kinana.


Akitoa salamu  za serikali  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene, licha ya kumshukuru Mwenyenzi Mungu kwa ajili ya maisha ya Mzee Zelothe, amesema kuwa, kupitia historia ya maisha ya Zelothe iliyoelezewa na watu wa makundi mbalimbali, inaonyesha wazi kuwa alikuwa ni mtu wa tofauti anayeweza kufananishwa na mtumishi wa Mungu na sio Polisi.


"Tumeshuhudia sura ya maisha ya Zelothe yaliyobeba dhamana nyingi ikiwemo baba, mlezi, mwalimu, kiongozi, Jemadari aliyewahudumia watu bila kujali hali za watu anaowahudumia, naweza kusema katika maisha yake ameandika hadithi nzuri,  ambayo kila mmoja anaweza kuihadithia" Amekiti Mhe. Simbachawene


Naye Mwenyekiti wa Wabunge wa mkoa wa Arusha na Naibu Waziri wa Madini Mhe. Steven Kiruswa ametoa pole kwa familia na kuelezea, msiba wa mzee Zelothe ni wa wana Arusha wote, Arusha imepoteza kiongozi hodari na makini, asiye na makundi mwenye kupenda kuunganisha watu bila kusita kusema ukweli pale inapostahili.


"Tumepoteza Mwenyekiti ambaye alitulea kwa upendo, alituunganisha wanachama, na mkoa ulitulia kisiasa, Zelothe ameondoka, tushirikiane na kuendela kumuomba Mungu atupe mtu sahihi kama Zelothe" Amesema Mhe. Kiruswa


Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mongella amesema kuwa, mkoa wa Arusha umepata pigo, kwa kupoteza kiongozi makini ambaye alipenda uwazi na uwajibikaji unao shirikisha watu kama timu,kiongozi ambaye hakuogopa kusema ukweli.


"Mimi binafsi alikuwa ni rafiki yangu na rafikii asiyetaka kitu kutoka kwa mtu ,zaidi asiyogopa kukwambia ukweli, kimsingi nilijifunza mambo mengi kutoka kwakwe ikiwemo maadili ya uongozi, tunaahidi kuyaenzi yote yaliyo mema" Amesema Mhe. Mongella.

Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa