WAANDISHI WA HABARI WANOLEWA KUHUSU MFUMO WA m – mama
Waratbu wa Mfumo wa dharura wa usafirishaji kwa kina mama wajawazito na watoto wachangaa (m-mama) Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro wametoa mafunzo kwa waandishi wa habari wa Mikoa hiyo ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuhakikisha Umma unapata elimu sahihi kuhusu matumizi sahihi ya mfumo huo unaolenga kunusuru vifo vitokanavyo na uzazi na kuipeleka kwa wananchi.
Mafunzo hayo yaliyofanyika mapema leo kwenye ukumbi wa Hotel ya New Safari iliyopo Mkoani Arusha, yalikuwa na lengo la kuwapatia waandishi wa habari wa redio za kijamii zilizo ndani ya Mikoa hiyo uelewa wa kina kuhusu mfumo huo wa dharura ulioanzishwa kwa ajili ya kusafirisha salama mama mjamzito na mtoto wakati inapotokea dharura.
Akifungua mafunzo hayo, kaiumu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Omary Chande amesema kuwa Serikali inatambua mchango wa Waandishi wa Habari katika kufikisha elimu sahihi kwa wananchi hivyo kupitia wao, elimu ya mfumo huo wa m-mama itawafikia wananchi kwa ufasaha.
“Ninawaomba mzingatie mafunzo haya ili mpate kuelewa nini kinapaswa kupelekwa kwa wananchi ili kuisaidia jitihada za Serikali za kupunguza au kumaliza kabisa vifo vya kina mama na watoto”. Amesisitza.
Kwa upende wake Muuguzi Mkuu na Mratibu wa Mfumo huo Mkoa wa Arusha, Getrude Anderson,amesema kuwa, mfumo huo umetengenezwa kuwa endelevu na nafuu kwa wananchi kupata fursa ya kupiga namba ya simu 115 bure ili kupata msaada wa haraka huku rufaa zaidi ya 90,000 zikiwa zimesafirishwa na zaidi vituo vya afya 7,600 vilichanganuliwa, sambamba na Serikali kuanzisha dawati la msaada mtandaoni kwa Mikoa ili kuripoti matatizo yoyote kuhusu m-mama.
Hata hivyo, waandishi hao wameipongeza Serikali kuendelea kuweka jitihada zaidi za kuhakikisha vifo vitokanavyo na uzazi vinapungua huku wakiahidi kuendelea kuunga mkono jitihada hizo kwa kutengeza vipndi mbalimbali vya kuelimisha umma kuhusu Mfumo huo.
Awali, Mfumo huo ulizinduliwa rasmi kwa awamu III ukijumuisha mikoa yote nchini huku awamu ya kwanza ikiwa mkoa wa Shinyanga na awamu ya pili Mikoa ya Mara, Arusha, Singida, Katavi, Iringa na Mtwara.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa