Wadau wa maendeleo kutoka shirika lisilo la Kiserikali la RENEAL INTERNATIIONAL EDUCATION OUTRICH wanaotekeleza mradi wa maabara za Kompyuta shule za Sekondari Nchini, Mradi unaowawezesha wanafunzi kusoma kwa njia ya TEHAMA kwa wepesi zaidi, wamefika Mkoani Arusha na Kupokelewa na Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Missaile Musa na kufanya mazungumzo mafupi ya kuendelea kuboresha mahusiano na kupanua wigo wa utekelezaji wa mradi huo.
Aidha, Wadau hao wameongozana na Afisa Tehama Kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na teknolojia ya Habari, David Nyangaka ambapo watakuwa Mkoani Arusha kwaajili ya kukagua maendeleo ya mradi huo.
Hata hivyo, Halmashauri 6 za Mkoa wa Arusha ni miongoni mwa halmashauri 28 Nchini zilizo nufaika na mradi huo.