Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, wametakiwa kufanya kazi kwa umoja na upendo.
Yamesemwa hayo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mheshimwa Idd Kimanta alipokuwa akizungumza na watumishi wote waliopo katika ofisi hiyo.
Amewataka kufanya kazi kwa bidii na kila mtu kwa nafasi yake ili kuleta maendeleo katika Mkoa mzima wa Arusha.
Aidha, amesisitiza zaidi kufanya kazi kwa amani huku wakifuata taratibu za utumishi wa umma.
Nae, Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha bwana Richard Kwitega amesema, yote yaliyozungumzwa na Mkuu wa Mkoa ni maelekezo kwa ajili ya watumishi wote kuyatekeleza kwa ufanisi mzuri wa kazi.
Akitoa neno kwa niaba ya watumishi wote bwana Sixbert Kihongole amesema, watafanya kazi kwa ushirikiano na upendo kwani hayo yote ni maelekezo kwa watumishi wote.
Nae, Elirehema Matoro amesema,maelekezo hayo ni nasaa nzuri kwa ujenzi wa maendeleo ya mkoa wa Arusha na hata pia katika kuongeza nguvu na hamasa ya kazi kwa watumishi.
Mheshimiwa Idd Kimanta alikutana na watumishi wa ofisi yake kwa lengo la kutoa maelekezo ya namna ya utendaji katika utumishi wa umma ili kuleta maendeleo na kutoa huduma nzuri kwa wananchi.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa