Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri zote saba za Mkoa wa Arusha, wametakiwa kuwawezesha watalamu wa wa Sekta za Maendeleo ya Jamii, Biashara na TEHAMA ili waweze kuwafikia wafanyabiashara na wamachinga kwa kuwapa elimu ya mikopo isyokuwa na riba na kuepukana na mikopo ya kaushadamu.
Rai hiyo imetolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Misaile Albano Mussa wakati akifungua Tamasha la wafanyabiashara ndogondogo Machinga mkoa huo, kongamano lenye lililowaunganisha wanyabiashara hao kwa lengo la kumshukuru Mhe.Raisi Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kulitambua kundi hilo na kuanza kuliwezesha kupitia mikopo yenye riba nafuu.
Amesema kuwa, watalamu hao wakiwezeshwa na kuwa na mkakati thabiti wa kutoa elimu kwa Wamachinga itafikia malengo ya kuwatambua na kuwaunganisha na fursa mbalimbali za kiuchumi, ikiwemo kuwa na sifa za kupata mikopo yenye riba nafuu na kuondokana na mikopo inayowaumiza wafanyabiashara hao na wengine kupoteza malengo yao ya kujikwamua kiuchumi.
"Nitoe wito kwa Wakurugenzi wa Halmashauri zote kuhakikisha wanafikia lengo la Serikali la kuwawezesha wamachinga kupata elimu ili kuwajengea uwezo na uelewa juu ya mikopo na uendeshaji wa biashara zao, jambo ambalo litaongeza kasi ya ukauji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwani mpaka sasa jumla ya wafanya biashara 224 waliochukua mkopo, ambao ni wachache kulinganisha na fedha zimetengwa, hivyo inahitajika nguvu ya ziada kuongeza idadi ya Wamachinga hao".Amesema Missaile.
Hata hivyo Wamachinga hao wamempongeza na kumshukuru Mhe.Rais kwa juhudi kubwa alizozifanya za kulitambua na kuliainisha kundi hilo bila kujali utofauti wa biashara zao, na kuwaunganisha na fursa za kibiashara sambana na kuwapatia mikopo yenye riba nafuu ambapo Serikali ya Dkt.Samia imetoa kiasi cha shilingi Bilioni 18.5 kwa Machinga nchi nzima huku Machinga wa mkoa wa Arusha ukipatwa wakipatiwa shilingi Million 501 kwa wamachinga na wafanya biashara wadogowadogo.
@arusha_district_council
@merudistrictcouncil2 @halmashauri_ya_karatu @longido.district_council @ngorongoro_dc @monduli_dc @ikulu_mawasiliano @ortamisemi
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa