• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

WANAFUNZI 45,682  WAPANGIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2024 MKOA WA ARUSHA...

Posted on: December 19th, 2023

Na Elinipa Lupembe


Jumla ya wanafunzi 45,682 wa mkoa wa Arusha, waliofaulu mtihani wa kuhitimu darasa la saba mwaka 2023, wamepangiwa kujiunga na kidato cha kwanza, kwenye shule za Serikali kwa mwaka ujao wa masomo 2024.


Akizungumza na mwandishi wetu, ofisini kwake, Afisa Elimu Mkoa wa Arusha, Mwl. Abel Adam Mtupwa, amesema kuwa, wanafunzi wote 45,682, wavulana ni 23,042 sawa na asilimia 50.4  na wasichana 22,640 sawa na asilimia 49.5,  waliofaulu mtihani wa kuhitimu darasa la saba mwaka 2023, wamepangiwa kujiunga na kidato cha kwanza kwenye, shule za Serikali, kwa mwaka wa masomo unaonza rasmi tarehe 08 Januari, 2024.


Amefafanuwa kuwa, kati yao wanafunzi 45,508, wavulana ni 22,374 na wasichana 23,134, sawa na asilimia 99.6, wamepangiwa shule za kutwa, wanafunzi 81 wamepangiwa shule za bweni za kawaida, wavulana 36 na wasichana 45, wanafunzi 35 wamepangiwa shule za vipaji maalum ambapo wavulana ni 20 na wasichana ni 15, huku wanafunzi 48 wakipangiwa kujiunga na vyuo vya ufundi wavulana 47 na wasichana 11.


Hata hivyo, Mwl. Mtupwa ameeleza historia ya wanafunzi hao kwamba, waliandikishwa kuanza darasa la kwanza mwaka 2017 wakiwa wanafunzi  57,609 na hadi kufikia mwaka 2023 walikuwa wanafunzi 54, 358 sawa na 94.3%.


Ameeleza kuwa, mwaka 2023 ufaulu katika mkoa wa Arusha, umefikia 86%, kwa wanafunzi 45,682 waliofaulu kutoka idadi ya wanafunzi 53,309, wavulana 25,863 na wasichana 27,448 waliosajiliwa na kufanya mtihani, kukiwa na ongezeko la 2% ukilinganisha na ufaulu wa jumla wa mwaka uliopita wa 2022 wa asilimia 84.


Aidha amewataka wazazi kuhakikisha wanawaandaa wanafunzi kuanza shule kwa kuwa Serikali inatoa elimu bila ada, na kuwakumbusha wazazi kuwaandaa watoto wote kuanza shule kwa wakati kwa kuwapa mahitaji yao binafsi kama waraka wa elimu unavyoelekeza.


"Serikali imekwishatekeleza majukumu yake, ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya madarasa, walimu na vitabu vya kiada na zaida pamoja na kutoa elimu bila ada, jukumu la wazazi ni kuwapa watoto wao mahitaji yao binafsi kama sare za shule, madaftari na kalamu, nauli za kwenda shule, pamoja na chakula cha mchana kwa wanafunzi waliopangiwa shule za kutwa kulingana na makubaliano kati ya wazazi na kamati za shule" Amewakumbusha wazazi.


Aidha amewasisitiza wazazi kuendelea kushirikiana na walimu na kuhakikisha wanafunzi wote wanaripoti shuleni kwa tarehe iliyopangwa na serikali sambamba na kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita ya kuhakikisha kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule anaoelekwa shule na kuoata elimu ili kufikia malengo ya serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Ikumbukwe kuwa, hii ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi Ibara ya 79 kifungu (g) ya kuhakikisha kila mtoto anapata elimu ya sekondari kwa kuongeza idadi ya wanafunzi wanaoendelea na kidato cha kwanza, kifungu  (h) Kuongeza uandikishaji wa wanafunzi katika Elimu ya Sekondari (i) kuongeza fursa za upatikanaji wa elimu ya sekondari kwa kuongeza idadi ya shule za sekondari nchini, Ilani ambayo imetekelezwa kwa vitendo mkoani Arusha.


Bofya Kiunganishi chini kuona shule walizopangiwa


https://www.tamisemi.go.tz/storage/app/allocations2023/allocations/2023/first-selection/arusha/index.html

Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa