• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

WANAFUNZI 5,298 KUFANYA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA MKOA WA ARUSHA 2024

Posted on: May 6th, 2024

Na Elinipa Lupembe


Jumla ya wanafunzi 5,298 mkoa wa Arusha, wanatarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu kidato cha sita unaoanza leo Mei 06, 2024 nchini, kwa mujibu wa ratiba ya Baraza la Mitihani la Taifa.


Akizungumza na mwandishi wetu, Afisa Elimu Mkoa wa Arusha, Mwl. Abel Mtupwa amesema kuwa, idadi hiyo ya wanafunzi, inajumuisha watahiniwa wa shule, watahiniwa wa kujitegemea pamoja na watahainiwa wa ualimu ngazi ya cheti na stashahada.


Amefafafanua kuwa kati ya watahiniwa 5,298, Watahiniwa 4,286 ni wa shule 'school candidates', watahiniwa 450 ni wa kujitegemea 'private candidates' na watahiniwa 562 ni wa Ualimu.


Mwl. Mtupwa amebainisha kuwa, watahiniwa wote watafanya mitihani yao, kwenye vituo rasmi 62  na vituo teule ni 23, huku kukiwa na kukiwa na jumla ya  wasimamizi wakuu 61 na wasimamizi wa Mikondo 135.


"Maandalizi yamekamilika kwenye vituo vya kufanyia mitihani, vifaa vyote vya muhimu vimepokelewa kwa utoshelevu wake kutoka Baraza la Mitihani la Tanzania na tayari  Semina elekezi kwa ajili ya kufanikisha kazi hii ya kitaifa zimefanyika kwa ufasaha kwa wasimamizi wote" Amesema Mwl. Mtupwa


Hata hivyo amewataka wasimamizi wote wa mitihani, kufanya kazi hiyo kwa uadilifu kwa kuzingatia kanuni, sheria na taratibu za mitihani ya Taifa, sambamba na kujiepusha na vitendo vinavyoweza kuathiri uendeshaji wa mitihani uliopangwa na Serikali, kwa kuwa tayari wanafunzi wameshaandaliwa vyema na walimu wao kwa shule zote.


Aidha, amewatakia kila la kheri watahiniwa wote na kuwataka kujiamini kwa kuwa mtihani huo hauna tofauti na mitihani mingine ambayo huwa wanaifa kipindi chote wawapo shuleni.


 Awaili mtihani wa kuhitimu kidato cha sita unaanza rasmi leo 06, Mei na unatarajiwa kumalizika terehe 24 Mei 2024

Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa