• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

WANANCHI KETUMBEINE WATAKIWA KUWA WATULIVU; SERIKALI IMEJIPANGA VEMA KUTATUA KERO ZAO.

Posted on: January 31st, 2024


Na Elinipa Lupembe.

Wananchi wa Tarafa ya Ketumbeine wilaya ya Longido, wametakiwa kuwa watulivu, na kujikita kwenye shughuli za maendeleo, kwa kuwa Serikali yao ya awamu ya sita, imejipanga vema kutatua kero na changamoto zinazowakabili, katika maeneo yao kisekta.


Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K Mongella, mara baada ya kupokea kero zinazowakabili wananchi hao, wakati wa mkutano wa Hadhara uliowakutani wakazi wa Tarafa ya Ketumbeine, uliofanyika kijiji cha Lopolosek.


Mhe. Mongella amesema kuwa, lengo la Serikali ya mama Samia ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma zote za msingi kwa kuzifikisha huduma hizo kwenye maeneo yao, huku kipaumbele cheke zaidi ni wananchi waishio maeneo ya vijijini.


Aidha, katika kutatua kero hizo, amemuagiza Mkuu wa wilaya hiyo kupitia ofisi ya Mkurugenzi, kujenga mara moja chumba cha kuhifadhia maiti kaatika kituo cha afya Ketumbeine, kwa kuwa, ukosefu wa Mochuari, unasababisha wananchi kuingia gharama kubwa kufuata huduma hiyo maeneo ya mbali, pindi wanawapoteza wapendwa wao na kumtaka  mkurugenzi kujenga choo kwenye soko la Ketumbeine ifikapo Machi 30, 2024 viwe vimekamilika.


Hata hivyo, Msimamizi wa Kitengo cha Matengenezo TANROAD Arusha, Injinia Reuben Jairo, amesema kuwa, fedha za usanifu wa barabara zimetengwa kwenye bajeti, wapo kwenye hatua za awali za kuandaa makabrasha kwa ajili ya kutengenza barabara hiyo kiwango cha lami kwa urefu wa Km 98 kutoka Longido - Oldonyolengai kuelekea  Ngorongoro, kama wananchi hao walivyoomba miaka miwili iliyopita.


Naye Meneja wa TARURA Wilaya ya Longido, Injinia  Laurence Msemo, amethibitihsa kuongezeka kwa bajeti ya barabara hadi kufikia bilioni 3.5, fedha ambazo zitawezesha matengenezo ya barabara zote za Longido kwa awamu, licha ya uharibifu unaotokana na mvua zinazoendelea kunyesha, huku akithibitisha kuomba bajeti ya ziada ya kufanya ukarabati wa barabara hizo.

Akijibu kero ya maji katika shule ya shikizi ya msingi Kale, Meneja wa RUWASA Wilaya ya Longido, amesema kuwa, mradi wa bilioni 1.3 unaotekelezwa kwenye kata ya Ketumbeini utahusisha maeneo yote ya kata hiyo na vijiji vyake licha ya kuwa ulichelewa kidogo katika utekelezaji wake.


Kuhusu suala la umeme wa REA kufikia vitongoji vitatu vya Kijiji hicho cha Lopolosek, Meneja wa REA wilaya ya Longido, amesema kuwa, mafundi wapo kazini wanaendelea na kazi ya za kusambaza umeme kwenye vitongoji baada ya kukamilisha usambazaji kwenye vijiji vyote.


Awali wananchi hao, waliwasilisha kero zao , ikiwemo ukosefu wa mochuari kituo chao cha afya, ukosefu wa choo soko la Ketumbeine, kutokufikiwa na

umeme baadhi ya vitongoji, ubovu wa barabara za ndani pamoja na uhaba wa maji unaosababisha mgao kijiji cha Kale


#ArushaFursaLukuki




                        
                       
                        </div>
                        <!-- /.right-sidebar-content -->
                        <!--/END RIGHT SIDEBAR CONTENTE SECTION-->
                    </div>



<div class=

Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa