Daktari wa Mifigo Mkoa wa Arusha Dk. Sabas Shange, amesema katika wiki hii ya uhamasishaji wa unywaji maziwa, wananchi wanatakiwa kuhakikisha wanakunywa lita moja ya maziwa kwa siku.
Ameyasema hayo katika mahojiano yake na kituo cha Television cha Star Tv katika wiki ya uhamasishaji wa unywaji maziwa.
Amesema, unywaji wa maziwa bora yaliyao chakatwa ni mazuri kwa afya ya binadamu kuliko kutumia maziwa ambayo hayaja chakatwa kwani yana hatari kubwa sana katika afya ya binadamu.
Pia, amewataka wafugaji kuhakikisha wanazalisha maziwa bora na kufuga mifugo iliyo bora ili iweze kuzalisha maziwa mengi.
Amewasisitiza wakulima kuhakikisha wanapata malisho bora kwa mifugo yao ili kuiwezesha mifugo kuwa bora na yenye tija katika kukuza uchumi wao.
Mkoa wa Arusha una jumla ya Ng’ombe takribani milioni 2 kati yao ng’ombe wa maziwa ni zaidi ya laki 2 na wenye uwezo kuzalisha lita 84,700 kwa siku na hivyo kuwawezesha wakulima kupata masoko ya uhakika katika viwanda vya usindikaji na vikundi mbalimbali.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa